Chadwick Boseman ashinda tuzo la Golden Globe

Marehemu Chadwick Boseman ameshinda tuzo hilo akiwa tayari amefariki na yeye ndiye muigizaji wa pili kuwahi kushinda tuzo hilo la muigizaji bora chini ya tuzo za Golden Globe kwa namna hiyo.

Ushindi huu unatokana na jukumu lake kwenye filamu kwa jina “Ma Rainey’s Black Bottom” ambayo ilikuwa kazi yake ya mwish kabla ya kifo chake.

Chadwick aliaga dunia tarehe 18 mwezi Agosti mwaka 2020 kutokana na saratani akiwa na umri wa miaka 43, kifo ambacho kilitikisa sekta ya filamu nchini Marekani kwa jina Hollywood.

Also Read
Jozi zote 666 za viatu vya shetani zimeuzwa!

Umaarufu wake ulitokana na kujumu lake kwenye filamu iitwayo “Black Panther” ambayo pia ilihisisha muigizaji wa nchi ya Kenya Lupita Nyong’o.

Akipokea tuzo hilo kwa niaba ya marehemu mume wake, Taylor Simone Ledward Boseman ambaye alijawa na hisia alisema kwamba Boseman angekuwepo kupokea tuzo hilo, angeshukuru Mungu, angeshukuru wazazi wake na mababu zake kwa mwongozo mzuri na kujitolea kwao na angeshukuru pia wote alioshirikiana nao kikazi.

Also Read
Kaburi La Pop Smoke Lavunjwa

“Angekuwa hapa angesema kitu kizuri, kitu cha kutia moyo, kitu ambacho kingepaaza sauti ndogo ambayo iko ndani ya kila mmoja wetu ambayo hutuambia kwamba tunaweza, hutuhimiza kuendelea kusonga mbele na kutuita turudi kwa mkondo unaostahili wakati huu kwenye historia.” aliendela kusema Bi. Taylor huku akibubujikwa na machozi.

Also Read
Tiffany Haddish kurudia vazi lake kwa mara ya tisa!

Alitaja baadhi ya waigizaji ambao walifanya kazi na marehemu mume wake. Tuzo hizo za Golden Globe ziliandaliwa kwa njia ya mtandao na nyota wote wa uigizaji walikuwa wakifuatilia matukio kutoka sehemu mbali mbali.

  

Latest posts

Mwelekezi Sir Jacob Otieno Ameaga Dunia

Marion Bosire

Daddy Owen Azindua Albamu Mpya

Marion Bosire

Ogopa Wasanii, Kibao Kipya Cha Willy Paul

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi