Far East Basketball Association yawatuza wachezaji bora

Chama cha Far East Basketball Association kimewatuza wachezaji basketiboli bora wa mwezi katika ligi za mashinani zikiwemo ile ya Street Inside exposure league (SIEL) na women Empowerment League(WEL) .

kulingana na tuzo hizo ,Sydney Chasimba ametawazwa mchezaji bora kutoka ligi ya SIEL north conference baada ya kuzoa pointi 116 katika mechi 4 na kuiwezesha klabu hiyo kushikilia nafasi ya pili huku Dereck Mcchemi akituzwa mchezaji bora wa North Conference baada ya kuisaidia timu yake kuipiku Lang’ata Worries alama 4-1

Also Read
Mourinho ateuliwa kocha wa AS Roma ya Italia kuanzia msimu ujao kwa miaka mitatu

Ligi ya SIEL inajumuisha timu 22 wakati ile ya WEL ikishirikisha timu 10 na kugawanywa kwa kanda mbili za north na South conference.

Mercy Wanjira -Meneja wa mipango kampuni ya Royal converters (kushoto) akiwa na washindi wa tuzo ya mchezaji na kocha bora wa mwezi  kwa vipusa

Maina Irungu wa Jericho Nets ametawazwa mchezaji bora wa Southern conference kwa kunyakua alama 111 na kuchangia kwa pointi nyingine 46 huku akiibuka bora kutoka ligi zote za North Conference na South conference .

Also Read
Mashindano ya msururu wa dunia katika raga ya wachezaji 7 upande HSBC kuanza Mei

Joseph Bondo akinyakua tuzo ya kocha bora wa mwezi kutoka Southern Conference .

Katika ligi ya Women Empowerement (WEL) Rose Mshila ameibuka kocha bora wa mwezi akiingoza timu yake ya Queens of the East kupata ushindi wa alama 3-1 ,naye Mary Sibweche akiibuka mchezaji bora katika ligi ya WEL akizoa alama 45 na rebounds 21 kwa timu yake ya Pack .

Also Read
Kogalo yakosa heshima ugenini Wundanyi na kupanda hadi nafasi ya tano ligi kuu FKF
Washindi wa tuzo ya mwezi ,wachezaji na makocha bora wakiwa na Bi Wanjira(katikati)

Kwenye hafla iliyoandaliwa mapema Ahamisi chama hicho kimeshirikiana na kampuni ya Royal Converters Limited kupitia kwa bidhaa yake ya Bella tissue kuwatuza wachezaji bora wa ligi hiyo ya mashinani katika mwezi uliopita.

Ushirikiano huo kati ya Far East Basketball Association na Royal Coverters kupitia kwa tissue ya Bella utadumu kwa miezi 6 ijayo ukilenga kuwainua na kuwapiga jeki wachezaji.

  

Latest posts

Police Fc washerehekea kurejea ligi kuu baada ya mwongo mmoja kwa dhifa

Dismas Otuke

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi