Chama cha FORD-Kenya chatangaza msimamo wa kuunga mkono BBI

Chama cha FORD-Kenya kimeelezea kujitolea kwake kuunga mkono ripoti ya mpango wa maridhiano wa BBI na kuapa kuwashawishi wafuasi wake kuunga  mkono utekelezaji wa ripoti hiyo.

Kiongozi wa chama hicho Moses Wetangula amesema hatua ya kuendeleza mbele mpango huo inatekelezwa na Wakenya.

Akiwahutubia wanahabari katika Kaunti za Kisii na Nyamira, Wetangula, ambaye pia ni Seneta wa Bungoma amewataka wafuasi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kwenye shughuli inayoendelea ya kukusanya saini kwa matayarisho ya kura ya maamuzi.

Also Read
Seneta Moi apeleka Rege ya BBI Pokot Magharibi

“Ripoti ya mwisho tuliyoiwekea saini huko KICC inaangazia matakwa ya Wakenya. Maswala mengi yenye utata na migawanyiko yametolewa na tuko na nakala itakayoleta ufanisi katika nchi hii,” amesema Wetangula.

Wetangula amesema ripoti ya mwisho ya BBI iliyozinduliwa katika Jumba la Mikutano ya Kimataifa, KICC,  itasaidia nchi hii kupiga hatua kubwa.

Also Read
Watu 36 waorodheshwa kwa wadhifa wa makamishna wa IEBC

Amesema matakwa ya chama hicho yamezingatiwa kwenye ripoti hiyo.

Wakati uo huo, baadhi ya wanasiasa kutoka eneo la Bonde la Ufa wameelezea kujitolea kwao kuunga mkono ripoti ya BBI.

Mbunge wa Nakuru Mashariki David Gikaria, mwenzake wa Gilgil Martha Wangari, Mbunge wa Njoro Charity Kathambi na Kimani Kuria wa Molo, wamesema mapendekezo ya kufanyia marekebisho katiba yatasuluhisha kasoro zilizopo.

Viongozi hao wamesema kesi za kupinga uchaguzi sasa zitasulihishwa kwa muda wa siku 30 badala ya 14 kama ilivyo kwa sasa, na kutoa nafazi ya kutosha kwa Mahakama kutathmini ukweli kabla ya kutoa uamuzi.

Also Read
Shule ya Msingi ya Uhuru yafungwa baada ya wanafunzi kuambukizwa korona

Hata hivyo, Mbunge wa Nakuru Magharibi Samuel Arama ametoa wito kwa viongozi kusoma ripoti hiyo kabla ya kutoa maoni yao kwa umma.

Wangari amesema mapendekezo kwenye ripoti hiyo yatawapiga jeki wanawake wanaotafuta uongozi.

  

Latest posts

Wafungwa watoroka katika gereza la Nanyuki usiku wa manane

Tom Mathinji

Visa 323 vipya vya COVID-19 vyathibitishwa hapa nchini

Tom Mathinji

Ujenzi wa reli kati ya Mai Mahiu na Longonot wakamilika

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi