Chama cha Jubilee chawatimua maseneta sita, Millicent Omanga, Issac Mwaura miongoni mwao

Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa chama cha Jubilee imewatimua maseneta sita maalum kutoka kwa chama hicho.

Kulingana na taarifa ya Katibu Mkuu wa chama hicho Raphael Tuju, maseneta hao waliotimuliwa mara moja ni Millicent Omanga, Isaac Mwaura, Mary Yiane, Naomi Jilo, Victor Prengei na Dekow Iman.

Also Read
Chama cha Jubilee kukosa mgombeaji katika uchaguzi mdogo wa Msambweni

Kamati hiyo imesema uamuzi huo umetokana na ripoti kutoka kwa kamati ya nidhamu ya chama cha Jubilee, baada ya maseneta hao kufika mbele yake na kujibu madai ya utovu wa nidhamu ya chama hicho.

Also Read
ANC chapongeza Jubilee kwa kujiondoa kwenye uchaguzi mdogo wa Matungu

Tuju amesema tayari uamuzi huo umewasilishwa kwa Spika wa Bunge la Seneti na Msajili wa vyama vya kisiasa.

Also Read
Serikali kutwaa silaha haramu kaskazini mwa nchi

Hata hivyo, maseneta hao wana haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi