Chama cha Moses Kuria chapigwa vita katika muungano wa UDA

Mzozo unatokota kwenye muungano wa United Democratic Alliance (UDA) unaohusishwa na Naibu Rais William Ruto kufuatia madai kwamba baadhi ya wanachama wa muungano huo hawajaridhishwa na chama cha Peoples Empowerment, chake mbunge wa Gatundu Kusini, Moses Kuria.

Also Read
Watu 388 waambukizwa COVID-19, wagonjwa sita waaga dunia

Duru zinadokeza kuwa migawanyiko imeanza kuibuka, huku kila tanzu la muungano huo likijaribu kujitafutia umaarufu.

Kuria amenukuliwa akisema baadhi ya viongozi wa muungano huo hawakufurahishwa na ushindi wa chama cha Peoples Empowerment kwenye uchaguzi mdogo wa hivi majuzi katika eneo bunge la Juja na wanapanga njama ya kukikandamiza.

Also Read
Ruto azitaka Idara za Polisi na Mahakama kujiepusha na mapendeleo ya kisiasa

Akiongea mjini Nyahururu, Kuria alisema chama hicho kitawasilisha wagombeaji katika chaguzi ndogo za eneo bunge la Kiambaa na wadi ya Muguga.

Also Read
Wazazi wahimizwa kuwa makini na watoto wao wakati huu shule zimefungwa

Hapo jana, Katibu Mkuu wa UDA, Veronica Maina, alitoa vyeti vya uteuzi kwa John Njuguna Wanjiku na Kamau Thumbi kuwania viti vya Kiambaa na Muguga mtawalia.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi