Chama cha PEP chajiondoa katika uchaguzi mdogo wa Kiambaa

Chama cha The People’s Empowerment Party (PEP) kimejiondoa kwenye uchaguzi mdogo eneo bunge la Kiambaa.

Kwenye ujumbe kupitia mtandao wa Facebook, mbunge wa Gatundu kusini Moses Kuria alisema chama hicho kiliafikia auamuzi lhuo baada ya majadiliano na chama cha UDA.

Chama hicho kilikuwa kimemteua Raymond Kuria kumenyana na mgombea wa chama cha UDA John Njuguna Wanjiku hali iliyokisiwa kuwa ingeleta migawanyiko kwenye muungano wa Husler.

Also Read
Raila: Ushauri wa Maraga wa kuvunja bunge umeweka nchi hii katika utata wa kikatiba

Kuria alisema chama cha PEP ni mwanachama na mshirika dau kwenye muungano wa Hustler, ikiwa ni pamoja na chama cha UDA kinachosimamiwa na aliyekuwa seneta Johnson Muthama, chama cha The Service Party kinachoongozwa na Mwangi Kiunjuri na vilevile chama cha PDP kinacoongozwa na Omingo Magara.

Also Read
Ruto awasuta wanaopinga mfumo wake wa kiuchumi

Kuria alisema chama hicho kwa sasa kinaangazia mpango wa kuimarisha umaarufu wake kote nchini kwa kuandaa ziara katika kaunti zote kukutana na wagombea watarajiwa kwa tiketi ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Also Read
Serikali yatakiwa kuharakisha usambazaji wa dawa za ARVs

Kiti cha eneo bunge la kiambaa kilibaki wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge Paul Koinange mnamo tarehe 31 mwezi machi mwaka huu.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi