Dozi 765,600 za chanjo aina ya AstraZeneca zawasili hapa nchini

Juhudi za kuhakikisha watu milioni 10 wanachanjwa dhidi ya Covid-19 hapa nchini, zilipigwa jeki Jumanne usiku baada ya taifa hili kupokea dozi 765,600 za chanjo aina ya AstraZeneca.

Akiwahutubia wanahabari baada ya kupokea shehena hiyo, mwenyekiti wa jopo kazi kuhusu usambazaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 katika wizara ya afya, Dkt. Willis Akhwale, alisema kuwa dozi hizo ambazo ni sehemu ya mpango wa usambazaji chanjo wa COVAX, zinatarajiwa kuimarisha juhudi zinazoendelea nchini za utoaji chanjo zinazolenga kuwapa chanjo watu milioni 10 kufikia mwisho wa mwaka huu.

Also Read
Visa 21 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

“Taifa hili lina karibu dozi milioni kumi za kukabiliana na Covid-19,  kwa hivyo tutaafikia lengo la kuwachanja watu milioni 10 kufikia mwishoni mwa mwaka huu jinsi alivyoahidi Rais Uhuru Kenyatta,” alisema Dkt  Akhwale.

Also Read
Washukiwa wawili wakamatwa kwa kuwawekea watu dawa katika vinywaji kabla kuwaibia

Dkt. Akhwale wakati huo huo alisema kuwa wizara ya afya kwa sasa inatathmini takwimu kuhusu matumizi ya chanjo ya Pfizer kwa watu wa umri wa kati ya miaka 16 na 18, na pia matumizi ya aina tofauti za chanjo kwa wanawake wajawazito.

Dkt. Akhwale alitoa wito kwa serikali za kaunti kuwahimiza wakenya kupata chanjo dhidi ya Covid-19 akisema nchi hii ingali inakabiliwa na hatari.

Also Read
Kenya ni ya tatu maskini zaidi kati ya mataifa yenye mapato ya kadri

Kenya imewachanja kikamilifu asilimia 82 ya wahudumu wa afya na asilimia 54 ya walimu huku Idadi ya waliichanjwa kikamilifu walio na umri wa miaka 50, ingali ni ya chini.

Kufikia sasa kaunti ya Nairobi imenakili asilimia kubwa zaidi ya chanjo zilizotolewa nchini ikifuatiwa na Nakuru, Kiambu na Taita Taveta.

  

Latest posts

Watu wawili wafariki baada ya jengo kuporomoka Kiambu

Tom Mathinji

TIFA: Uwaniaji Urais wa Raila-Karua ni maarufu zaidi

Tom Mathinji

Tofauti za kisiasa miongoni mwa viongozi wa Ukambani zachacha

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi