Chanjo milioni moja dhidi ya korona kuwasili Kenya leo

Chanjo za kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 zitaanza kuwasili humu nchini leo kupitia mpango wa Covax.

Kulingana na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, Kenya itapokea dozi milioni 1.02 za chanjo za Oxford/Astrazeneca.

Amesema dozi  hizo milioni 1.02 ni za kwanza kati ya dozi milioni 4.1 zinazotarajiwa hivi karibuni, huku taifa hili likitarajia kupokea jumla ya dozi milioni 24.

Also Read
Kanisa Katoliki: Ghasia za Laikipia zilichochewa kisiasa

Kagwe, ambaye alizungumza huko Nyeri siku ya Jumapili, alisema wahudumu wa afya katika kaunti zote 47 watapewa kipau mbele kwenye chanjo hiyo.

Also Read
Maambukizi ya Covid-19 yanazidi kuongezeka huku watu 442 zaidi wakiambukizwa nchini

Wafanyikazi wengine walio mstari wa mbele kama vile walimu na maafisa wa usalama pia wako kwenye orodha ya watakaopokea chanjo hiyo mwanzo.

Also Read
Maambukizi ya COVID-19 yaendelea kuongezeka huku visa vipya 604 vikiripotiwa

Hata hivyo Waziri Kagwe ameonya kwamba kuwasili kwa chanjo hizo hakufai kuwa sababu ya Wakenya kukaidi kanuni za kuzui msambao wa virusi vya korona, akihoji kwamba ulimwengu haujaweza kuzalisha chanjo za kutosha.

  

Latest posts

Nyongeza ya bei za mafuta yapingwa Mahakamani

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Tom Mathinji

Wazazi wasema watatetea mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi