Chebet na Jebitok wafuzu fainali ya mita 1500 michezo ya jumuiya ya madola

Wakenya Ednah Jebitok na  Winnie Chebet wamefuzu kwa fainali ya mita 1,500 Ijumaa  katika siku ya nane ya michezo ya jumuiya ya madola mjini Birmingham Uingereza.

Jebitok alimaliza wa tatu katika mchujo wa kwanza wa raundi ya kwanza kwa  dakika  4 sekunde 13 nukta 84,nyuma ya  Ciana Mageean wa Ireland Kaskazini na Abbey Caldwell waliochukua nafasi za kwanza na pili mtawalia.

Also Read
Wanariadha zaidi ya 400 kuhudhuria majaribio ya kitaifa kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20
Also Read
Omanyala afuzu kwa nusu fainali ya mita 100 michezo ya jumuiya ya Madola

Bingwa wa Afrika ,Winnie Chebet pia aliwahi tiketi ya fainali,  baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu  katika mchujo  pili kwa kutumia dakika 4 sekunde 16 nukta 11.

Also Read
Jebitok ashinda makala ya 41 ya Cross Internacional de Venta de Banos

Winnie Nanyondo wa Uganda aliongoza akifuatwa na Katie Snowden  wa Uingereza.

Fainali ya shindano hilo itaandaliwa Jumapili usiku ambayo ni siku ya mwisho ya mashindano.

  

Latest posts

Gonzalo Higuain astaafu rasmi kutoka soka

Dismas Otuke

Takwimu za kipute cha 22 cha kombe la dunia nchini Qatar

Dismas Otuke

Sharon Chepchumba atua Ugiriki kupiga Voliboli ya kulipwa kwa miezi sita

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi