Chebet na Rono watwaa ubingwa wa mbio za nyika Nairobi

Emily Chebet amestahimili ukinzani mkali kutola Winfred Mtile  Yavi wa Bahrain , na kutwaa ushindi wa mbio za kilomita 10 kwenye  mashindano ya  mbio za nyika ukanda wa Nairob, i   katika  uwanja wa idara ya magereza mtaani  Nairobi West  mapema Jumamosi.

Chebet amekata utepe kwa dakika 32 sekunde 13 nukta 1,akifuatwa na Yavi kwa dakika 32 sekunde  23 nukta 7 huku  Mercy Chepkorir kutoka  Lang’ata akiambulia nafasi ya tatu kwa dakika 33 sekunde 3 nukta 8.

Also Read
Serikali ya Uingereza yaidhinisha uuzaji wa klabu ya Chelsea kwa pauni bilioni 4 nukta 25
Chebet akiongoza kilomita 10

Katika  mbio za Wanaume kilomita 10,  Geofrey Rono kutoka Lang’ata alimaliza wa kwanza kwa dakika 27 sekunde 49 nukta 1 akifuatwa na Musa Mitei wa Dagoretti kwa dakika 27 ,sekunde 56 nukta 1 .

Also Read
Oooh Nyumbani ni nyumbani David Ouma ateuliwa naibu kocha wa SOFAPAKA miaka 8 baade

Dennis Kipkirui na Florence Chepkoech wameshinda mbio za kilomita 8 na  6  kwa wanaume na wasichana chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 mtawalia.

Kipkirui ameshinda mbio za kilomita 8 wavulana kwa muda wa dakika 22 sekunde 49 nukta 2 akifuatwa na Nehemiah Kipyegon aliyetumia dakika 25 sekunde 59 nukta 6 katika nafasi ya pili ilihali Peter Kibui akaridhia nafasi ya tatu kwa dakika 23 na sekunde 3.

Also Read
Brimin Kipkorir na Agnes Barsosio watwaa ubingwa wa makaka ya kwanza ya Nairobi Marathon

Kaunti ya Nairobi imeteua kikois kitakachoshiriki mashindano ya kitaifa ya mbio za Nyika Jumamosi ijayo katika kijiji cha Lobo mjini Eldoret.

  

Latest posts

Ronaldo kuachiliwa kuondoka Old Traford

Dismas Otuke

Manara na Hersi Matatani

Marion Bosire

Mary Moraa Bingwa wa Mita 800 kwa Wanawake Kwenye Michezo ya Jumuia ya Madola Mwaka 2022

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi