Chebukati atetea gharama ya kuandaa kura ya maamuzi ya shilingi bilioni 14

Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka hapa nchini-IEBC Wafula Chebukati ametetea makisio ya tume hiyo kuhusu gharama ya kuandaa kura ya maamuzi ya shilingi bilioni-14.

Kwenye taarifa, Chebukati alisema kwamba kiwango hicho kinatokana na data za kihistoria na ufahamu wa tume hiyo katika kusimamia uchaguzi hapa nchini.

Also Read
George Koimburi ndiye mbunge mpya wa Juja

Aidha alisema matamshi ya kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga kwamba kura ya maamuzi haifai kuwagharimu walipaji kura zaidi ya shilingi bilioni-2, sio sawa na hayaangazii hali halisi ya chaguzi.

Kiongozi huyo wa ODM alidai kwamba gharama ya kila mpigaji kura katika mataifa yanayoandaa chaguzi mara kwa mara, ni kati ya shilingi 100 na 200, na hivyo hakuna haja kutumia kiasi kikubwa cha fedha kinachopendekezwa na tume ya IEBC.

Also Read
IEBC yaidhinisha mswada wa BBI

Hata hivyo Chebukati alisema kwamba Kenya ilipoandaa kura ya maamuzi ya mwaka 2010, gharama ya kila mpigaji kura ilikuwa shilingi 794.

Vile vile alitoa mfano wa duru ya pili ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2017, ambayo alisema iliigharimu nchi hii shilingi bilioni 12.

Also Read
Mutyambai aamuru uchunguzi kuhusu ghasia za Murang’a

Mkuu huyo wa tume ya IEBC alisema kwamba wataandaa bajeti ya kina ili kukaguliwa na kuidhinishwa tume hiyo ikipokea arifa ya kuandaa kura ya maamuzi.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi