Chepkemoi na Chebolei watwaa ubingwa wa kilomita 10, mbio za nyika mwaka 2022

Joyce Chepkemoi  na Samuel Chebolei ndio mabingwa wa mwaka 2022 wa mbio za nyika kwenye mashindano yaliyoandaliwa Jumamosi eneo la Lobo village mjini Eldoret.

Chebolei aliyekuwa akishiriki mbio za kilomita 10 kwa watu wazima kwa mara ya kwanza akitoka North Rift ,alikistahimili ukinzani mkali na kutwaa ushindi kwa dakika 29 sekunde 28 nukta 9.

Samuel Chebolei akikata utepe mbio za kilomita 10

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Kennedy Kiprop kutoka mkoa wa magharibi kwa dakika 29 sekunde 35 nukta 2 ,naye Vincent Kiprotich wa Central Rift kwa dakika 30 sekunde 2 nukta 6.

Also Read
Brimin Kipkorir na Agnes Barsosio watwaa ubingwa wa makaka ya kwanza ya Nairobi Marathon

Joyce Chepkomoi kutoka KDF kwa dakika 34 akifuatwa na Margaret Chelimo kutoka huduma ya kitaifa ya Polisi kwa dakika 34 sekunde 1 nukta 8 ,huku Celphine Chespol wa magereza , akiridhia nafasi ya tatu kwa dakika 34 sekunde 23 nukta 3.

Also Read
Majaribio ya kitaifa ya mbio za kupokezana kijiti yaahirishwa
Joyce Chepkemoi akiibuka mshindi wa mbio za kilomita 10 wanawake

Benson Kiplagat na Faith Cherotich wote kutoka South Rift , walitawazwa mabingwa katika kitengo cha chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20.

Kiplagat alikata utepe katika kilomita 8 kwa dakika 24 na sekunde 8, akifuatwa na Samuel Kibathi wa Central kwa dakika 24 sekunde 16 nukta 9, wakati Raynind Kipkorir wa South Rift akichukua nafasi ya tatu kwa dakika 24 sekunde 21 nukta 4.

Also Read
Wanariadha chipukizi 80 watakaochaguliwa kuingia kambini kubainika wiki hii
Benson Kiplagat akishinda kilomita 8 wavulana

Cherotich ameshinda mbio za wasichana kilomita 6 ,akiziparakasa kwa dakika 20 sekunde 28 nukta 4 ,akifuatwa na Purity Chepkurui wa South Rift kwa dakika 20 sekunde 34 nukta 8,  naye Grace Loibach kutoka Central Rift akimaliza wa tatu kwa dakika 21 na sekunde 7.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi