Cheruiyot alenga kutetea taji ya dunia ya mita 1500 mjini Oregon USA

Bingwa wa dunia katika mbio za mita 1500 Timothy Cheruiyot amesema licha kupanga kushiriki mashindano mengi mwaka huu,lengo lake kuu litakuwa kutetea dhahabu ya mita 1500 kwenye mashidnano ya dunia yatakayoandaliwa mjini Oregon Marekani baina ya Julai 15 na 24 .

Kwenye mahojiano na KBC kwa njia ya kipekee ,Cheruiyot ambaye pia ni mshindi wa nishani ya fedha ya Olimpiki ,amesema anaendelea vyema na mazoezi huku akipanga kuiwakilisha timu yake ya magereza ya mbio za nyika za kupokezana kijiti wakati wa mashindnao ya kitaifa ya mbio za Nyika mjini Eldoret tarehe 22 mwezi huu.

Also Read
Muneria na Chespol watawazwa mabingwa mbio za nyika za magereza

Cheruiyot aliye na umri wa miaka 26, amesema atakuwa akishiriki mbio za kitaifa za nyika ili kutatufa kasi,kabla ya kuanza kwa msimu wa Diamond league mwezi Mei , ambapo pia atawinda kutetea taji aliyotwaa mwaka uliopita .

Also Read
Cheruiyot kuwania tuzo ya mwanariadha bora wa mwaka
Cheruiyot akishindana mita 1500 katika michezo ya Olimpiki mjini Tokyo Japan mwaka uliopita

“Nitashiriki mashindano ya kitaifa ya mbio za nyika mjini Eldoret , kutafuta kasi ,baada ya kurejea mazoezini ,lakini mwaka huu my main target ni kudefend tittle yangu katika mashindano ya dunia”akasema Cheruiyot

Also Read
Faith Kipyegon asajili muda wa nne wa kasi duniani katika mita 1500

“Mwaka huu kuna mashindano mengi napanga kushiriki lakini ,mwanzo kabisa nataka nidefend title yangu then nitashiriki Commonwealth games najua haitakuwa rahisi lakini niko tayari”akaongeza Cheruiyot.

Kikosi cha magereza kimeripoti kambini Jumanne kujiandaa kwa majaribio ya kitaifa ya mbio za nyika mjini Eldoret.

  

Latest posts

Riadha Kenya kuandaa seminaa kwa wanariadha Januari 21 kutangulia mashindano ya kitaifa

Dismas Otuke

Polisi wachunguza mauaji ya mwanamke aliyepatikana ndani ya sanduku

Tom Mathinji

Kenya haitatuma timu kwa michezo ya Olimpiki ya majira ya Baridi Beijing

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi