Cheruiyot, Simotwo na Kipsang kushiriki nusu fainali ya mita 1500

Bingwa wa dunia Timothy Cheruiyot na Charles Simotwo ,watashiriki mchujo wa kwanza wa nusu fainali ya mita 1500 katika michezo ya Olimpiki mjini Tokyo Japan Alhamisi jioni.

Also Read
AIU yalenga kupima sampuli zaidi ya 800 katika michezo ya Olimpiki ya mwaka huu

Mchujo huo utaanza saa nane adhuhuri majira ya Afrika mashariki ukifuatwa ule wa pili utakaomshirikisha Abel Kipsang.Kenya haijashinda dhahabu ya Olimpiki katika shindano hilo tangu mwaka 2008 mjini Beijing China kupitia kwa Asbel Kiprop.

Also Read
Rais wa zamani wa shirikisho la riadha duniani Lamine Diack afungwa miaka miwili gerezani
Wanariadha watano bora kutoka kila mchujo na wawili watakaosajili muda wa kasi kutoka michujo yote wakifuzu kushiriki fainali ya Jumamosi.

Kenya imezoa medali tano zote kupitia riadha kufikia sasa dhahabu ya mita 800 yake Emmanuel Korir, fedha 2 zao Hellen Obiri katika mita 5,000 na Ferguson Rotich katika mita 800.

Also Read
Watu 36 zaidi wafariki kutokana na COVID-19 hapa nchini

Medali zote za shaba zimetwaliwa katika mita 3,000 kuruka viunzi na maji kupitia kwa Benjamin Kigen na Hyvin Kiyeng.

  

Latest posts

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

NCIC kuwatumia vijana kuwa mabalozi wa amani kabla ya msimu wa uchaguzi

Tom Mathinji

Tusker ,Gor Mahia kufungua pazia kwa mechi ya Super Cup Jumatano

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi