China inaendelea na juhudi za kuleta maendeleo yasiyochafua mazingira barani Afrika

China itaendelea kuziunga mkono nchi zinazoendelea kuendeleza nishati safi inayotoa kiwango kidogo cha kaboni, na haitajenga miradi mipya ya umeme wa makaa ya mawe nje ya nchi. Ahadi hii iliyotolewa na rais Xi Jinping wa China kwenye mjadala mkuu wa kikao cha 76 cha Baraza Kuu wa Umoja wa Mataifa imeonesha tena nia thabiti ya China kuendeleza nishati mbadala kimataifa.

Katika miaka ya hivi karibuni, athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa kwa bara la Afrika zimeongezeka kadri siku zinavyokwenda, na yamekuwa “mwuaji asiyeonekana” wa kundi la wanyonge.  Mwaka 2019, kimbunga kiitwacho Idai kiliikumba pwani ya Afrika mashariki na kusini, na kusababisha watu karibu laki 2 kukimbia makazi yao, na kuharibu eneo la hekta laki 7.8 la mazao ya kilimo, na mwaka huohuo, Pembe ya Afrika ilikumbwa na mvua kubwa baada ya ukame wa mwaka mmoja na kusababisha mafuriko na maporomoko ya udongo, hali ambayo iliweka mazingira ya kuzaliana kwa nzige, na hatimaye balaa kubwa la nzige likatokea mwaka uliofuata wa 2020. Mapema mwezi huu, theluji ilianguka ghafla katika nchi ya Ikweta Cameroon na kusababisha uharibifu kwa sekta ya kilimo……

Wanasayansi wamekubaliana kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanatokana na shughuli za kibinadamu zinazotoa hewa zinazosababisha ongezeko la joto, kwa neno jingine hewa ya kaboni.
Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika imetaja kuinua uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kutimiza maendeleo endelevu kama moja ya malengo makuu. Hivi sasa, nchi za Afrika zinajitahidi kuhakikisha nishati kuwa safi, kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni, na kutafuta maendeleo endelevu na jumuishi ya kiuchumi yanayotoa kiwango kidogo cha kaboni.

Also Read
Hatua za China za kuleta amani na mshikamano hazipaswi kuchukuliwa kuwa ukandamizaji wa kidini au kikabila

China ni mwenzi mkubwa wa maendeleo endelevu ya kijani barani Afrika. Mapema mwaka 2015, China ilitaja “kijani” kwenye utaratibu wa ushirikiano wa kilimo kati yake na Afrika, na kutoa mpango wa kuunga mkono Afrika kutekeleza miradi 100 inayohusu nishati safi, ulinzi wa wanyamapori, kilimo rafiki kwa mazingira, na ujenzi wa miji ya akili bandia.

Kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika mjini Beijing mwaka 2018, China iliahidi tena kuzisaidia nchi za Afrika kujenga miradi 50 ya maendeleo ya kijani na ulinzi wa mazingira, na pia kuunganisha pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na ushirikiano wa China na Afrika ili kuhimiza maendeleo ya kijani ya ushirikiano wao.

Mwezi Septemba mwaka jana, China ilitoa ahadi ya kutimiza malengo mawili makubwa ya “kufanya utoaji wa kaboni kufikia kilele chake” na “kusawazisha utoaji na uvutaji wa kaboni”, kuhimiza ushirikiano wa kimataifa wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kujenga “Ukanda na Njia” kuwa ya kijani.

Also Read
Juhudi za miaka 100 za CPC zina maana gani kwa nchi za Afrika?

Afrika ina watu zaidi ya bilioni 1.2, na nusu ya ardhi yake haijafikiwa na umeme. Lakini kadri teknolojia ya nishati safi kama vile jua, upepo na maji inavyozidi kutumiwa katika kuzalisha umeme, tatizo la upatikanaji wa umeme linatatuliwa siku hadi siku. Takwimu zimeonesha kuwa tokea mwaka 2010, miradi iliyojengwa na China imechangia theluthi moja ya ongezeko jipya la umeme barani Afrika.

Sera ya China kuunga mkono maendeleo ya kijani ya Afrika inatekelezwa kwa vitendo na kuwa mradi wa umeme wa jua mjini Garissa, Kenya, bwawa la kuzalisha umeme wa maji la Karuma, Uganda, mradi wa umeme wa upepo mjini Adama, Ethiopia na miundombinu mingine mikubwa. Kwa mujibu wa Shirika la Nishati la Kimataifa IEA, China inajenga miradi ya kuzalisha umeme katika nchi 24 zilizo kusini mwa Sahara barani Afrika, na inatarajiwa kuwa miradi 49 ya kuzalisha umeme itakamilika kabla ya mwaka 2024, na kati yake mingi ni miradi ya nishati mbadala.

Katika kitabu cha “mabadiliko ya hali ya hewa, athari na mazoea”, mtunzi wake Michael Adani alisema China inajenga uhusiano wa kiwenzi na nchi za Afrika kupitia mapendekezo kama vile “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na kuzisaidia kupata maliasili, miundombinu na teknolojia zinazohitajika, ili kukabiliana vizuri na msukosuko wa mabadiliko ya hali ya hewa.

Also Read
China yafutilia mbali madeni yasiyo na riba kwa mataifa 15 barani Afrika

Kuhakikisha kila mtu anapata nishati safi ya bei nafuu uhakika na uendelevu ni msingi wa maendeleo ya Afrika, na pia ni moja ya malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa. Mchango wa Afrika kwa utoaji wa hewa zinazosababisha ongezeko la joto duniani ni mdogo sana ikilinganishwa na sehemu nyingine, lakini athari ilizopata ni kubwa mno.

Afrika inapaswa kujiunga na mpito wa nishati duniani, lakini haina haja ya kupitia kila kipindi cha maendeleo ya teknolojia, kwani inaweza kupata teknolojia mpya nzuri sokoni na kutoa fumbuzi muhimu kwa kuendeleza nishati mpya. Afrika ya sasa inakabiliwa na changamoto mbili, moja ya janga la COVID-19 na nyingine ni hali ya kuwa nyuma kimaendeleo ambayo imekuwepo kwa miaka mingi.

China itaendelea kuziunga mkono nchi za Afrika kuendeleza uchumi unaotoa kiwango kidogo cha kaboni na kuhimiza mageuzi ya nishati mbadala, ili kuchangia ufufukaji wa uchumi wa kijani wa nchi mbalimbali.

Na Hassan Zhou

  

Latest posts

Watu 20 wauawa na wanamgambo katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo

Tom Mathinji

Rais Joe Biden apona virusi vya Covid-19

Tom Mathinji

Manara na Hersi Matatani

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi