China kusaidia mataifa mengine kukabiliana na Covid-19

China inasema imejitolea kuzisaidia nchi nyingine kukabiliana na janga la COVID-19, ikikariri kwamba imetoa usaidizi kuhusiana janga hilo kwa nchi 69 na mashirika mawili ya kimataifa.

Kwenye taarifa maafisa walisema China pia itatoa misaada ya chanjo kwa nchi 28.

Taifa la hivi punde ambalo limepokea chanjo cha ugonjwa wa COVID-19 kutoka china ni Guinea.

Also Read
Watu 54 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Kulingana na mwanachama wa baraza la ushauri wa kisayansi la serikali ya Uturuki, chanjo ya ugonjwa wa COVID 19 ilyotengenezwa na China Sinovac Biotech ina uwezo wa asilimia 83. 5 wa kuzuia maambukizi.

Hayo ni kulingana na matokeo ya mwisho ya awamu ya tatu ya kufanyia chanjo hiyo majaribio na pia ina uwezo wa asilimia 100 wa kuzuia maambukizi ya maradhi sugu.

Also Read
Tundu Lissu: Uchaguzi mkuu wa Tanzania ulikumbwa na udanyanyifu

Kadhalika chanjo ya kuzuia maambukizi ya virusi aina ya adenovirua iliyotengenezwa na kampuni ya CanSino Biologics ina uwezo wa asilimia 90.9 ya kuzuia maambukizi ya maradhi sugu.

Also Read
Ni mwanafunzi mmoja aliyeambukizwa covid-19 tangu kufunguliwa kwa shule

Pia ina uwezo wa asilimia 65.7 wa kuzuia dalili za maambukizi ya ugonjwa wa COVID19 baada ya mgonjwa kupokea chanjo mmoja.

Chanjo ya virusi aina ya adenovirus kulingana na China inatarajiwa kumpa mtu kinga kwa miaka miwili.

  

Latest posts

Mwanaume mmoja ashtakiwa kwa makosa saba ya mauaji Marekani

Tom Mathinji

Uganda yaidhinisha Kiswahili kuwa Lugha rasmi

Tom Mathinji

Walinda usalama wawili wa Umoja wa Mataifa wauawa nchini Mali

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi