China yaendelea kuzibeba nchi za Afrika na nyingine kwenye sekta ya kilimo

Na Fadhili Mpunji

Serikali ya China imetangaza hivi karibuni kuwa kuanzia mwezi Septemba mwaka huu itaondoa kabisa ushuru kwenye asilimia 98 ya bidhaa za kilimo kutoka nchi 16 zenye mapato ya chini, tisa ya nchi hizo zikiwa ni nchi za Afrika.

Hatua hii ni mwendelezo wa hatua kama hiyo iliyochukuliwa kwenye mkutano wa tatu wa mawaziri wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika wa mwaka 2006, uliotangaza kuruhusu bidhaa 440 kutoka nchi za Afrika zilizo nyuma zaidi kimaendeleo.

Taarifa iliyotolewa mwanzoni mwa mwezi Agosti na wizara ya fedha ya China imezitaja Guinea, Djibouti, Mozambique, Rwanda, Sudan, Togo, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Eritrea na Chad kuwa ni nchi za Afrika zitakazonufaika na mpango huo, na Cambodia, Kiribati, Laos, Nepal, na visiwa vya Solomon Islands kuwa ni nchi za Asia zitakazonufaika na utaratibu huo.

Also Read
kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Mali Kanali Assimi Goïta atangazwa Rais

Kwa wanaofuatilia kwa karibu uhusiano kati ya China na nchi za Afrika, au hata nchi nyingine zilizo nyuma kimaendeleo, wanaweza kukumbuka kuwa China imekuwa ikirudia mara kwa mara kuwa itajitahidi kufanya maendeleo yake yanizufaishe nchi nyingine. Taarifa iliyotolewa na wizara ya fedha ya China ni ushahidi kuwa China inatekeleza kivitendo ahadi hiyo.

Inatakiwa ikumbukwe kwamba dunia kwa sasa inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kupungua kwa mapato ya nchi nyingi zinazotegemea uuzaji wa bidhaa zake nje ya nchi, hasa bidhaa za kilimo. Uamuzi wa China umekuwa kwa wakati mzuri kwa nchi hizo za Afrika ambazo zinategemea sekta ya kilimo. Ingawa utekelezaji wa hatua ya kufuta ushuru kwa bidhaa zinazoingia China huwa inatekelezwa hatua kwa hatua kwa kufuata vigezo vya karantini na ukaguzi, mchakato wake si mgumu na mara nyingi utekelezaji wa mchakato huo pia ni eneo lingine ambalo ni fursa ya ushirikiano.

Also Read
Jamaa Akabiliwa na Kifungo Gerezani kwa Kukabidhi Mwanawe Bunduki Aliyotumia Kuua Watu Wanne

Tunatakiwa kukumbuka pia kuwa sekta ya kilimo ni sekta inayogusa watu wengi zaidi wa Afrika, na ni sekta ambayo ni uti wa mgongo kwa nchi nyingi za Afrika. China inapotangaza fursa ya kuruhusu bidhaa za kilimo kutoka nchi za Afrika kuingia kwenye soko lake bila ushuru, ni njia ya dhati yenye lengo la kuwaunga mkono wakulima wengi wa nchi za Afrika, ambao mara nyingi kilio chao kikubwa kimekuwa ni ukosefu wa soko la mazao yao.

Nchi za Afrika zina hali tofauti za kijiografia, na si nchi zote zina mazingira yanayofaa kwa mazao yote ya kilimo, kuna nchi zenye mazingira yanayofaa kwa kilimo cha mazao ya mizizi kama muhogo na viazi, kuna nchi zenye mazingira yanayofaa kwa kilimo cha mazao ya mikunde kama vile maharage, soya, choroko nk, kwa hiyo China inapotoa fursa ya asilimia 98 kimsingi ni karibu mazao yote yanayozalishwa katika nchi zilizotajwa.

Also Read
Samoa yamuapisha Waziri mkuu wa kwanza mwanamke katika hali tatanishi

Hata hivyo kumekuwa na changamoto ya kutumia fursa hiyo ipasavyo. Licha ya fursa hiyo kutolewa kwa nchi nyingi za Afrika, kukidhi wingi wa kiasi kinachoagizwa na vigezo vya karantini imekuwa ni changamoto kwa wauzaji wengi. Hili ni jukumu la wakulima, wafanyabiashara na serikali za nchi za Afrika kuhakikisha wanajipanga vizuri ili kutumia fursa hii.

  

Latest posts

Boro wamtimua meneja Chris Wilder kwa matokeo duni

Dismas Otuke

Marekani kutatua mzozo wa mpakani baina ya Israel na Lebanon

Tom Mathinji

Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi Burkina Faso Paul-Henri Damiba ajiuzulu

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi