China yafutilia mbali madeni yasiyo na riba kwa mataifa 15 barani Afrika

China imetia saini makubaliano ya kuahirisha madeni na mataifa 12 ya kiafrika, na kuondolea mbali mikopo isiyo na riba, ambayo muda wake wa malipo ungeanza mwaka huu kwa mataifa 15 barani Afrika.

Maafisa wa nchi hiyo wanasema uamuzi huo uliafikiwa chini ya mpango wa kuahirisha mikopo wa kundi la mataifa 20 yenye uwezo mkubwa duniani, ili kuyasaidia mataifa kujinusuru na athari za janga la COVID-19.

Also Read
Baadhi ya Maseneta Marekani wadinda kuidhinisha ushindi wa Biden

Uhusiano wa kibiashara kati ya China na bara Afrika, ulifikia kiasi cha dolla bilioni 150 katika miezi kumi ya kwanza mwaka huu.

Maafisa wa serikali ya China walisema nchi hiyo ilitumia zaidi ya dola bilioni 60 ambazo ni sawa na asilimia 70 ya usaidizi wa kifedha ambao uliahidiwa kwenye mkutano wa Beijing wa kongamano la ushirikiano kati ya China na bara Afrika mwaka wa 2018.

Also Read
Ushawishi wa China barani Afrika watokana na ushirikiano wa dhati kati ya pande hizo mbili

Maafisa waliohudhuria mkutano huko wa Beijing walisema fedha hizo zilitumiwa kwa miradi mikubwa ambapo baadhi ya miradi hiyo imekamilishwa na mingine ingali inatekelezwa.

Also Read
Alassane Ouattara achaguliwa tena kuiongoza Ivory Coast

Miradi hiyo ni pamoja na awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli kutoka Nairobi hadi Malaba na daraja linalounganisha jiji la Maputo na Katembe nchini Msumbiji.

  

Latest posts

Boro wamtimua meneja Chris Wilder kwa matokeo duni

Dismas Otuke

Marekani kutatua mzozo wa mpakani baina ya Israel na Lebanon

Tom Mathinji

Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi Burkina Faso Paul-Henri Damiba ajiuzulu

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi