China yarusha makombora 11 karibu na kisiwa cha Taiwan

Uchina imerusha makombora kadhaa karibu na Taiwan katika mojawapo ya mazoezi yake makubwa ya kijeshi katika eneo la Taiwan Strait, siku moja baada ya spika wa bunge la uwakilishi nchini Marekani Nancy Pelosi kuzuru kisiwa kinachojitawala cha Taiwan.

Uchina imerusha makambora 11 katika bahari zilizoko karibu maeneo ya kaskazini mashariki na kusini magharibi mwa pwani ya Taiwan katika mazoezi yalioanza mchana.

Also Read
Magufuli ampongeza Waziri wa China kwa kutovalia barakoa

Uchina inadai kuwa bahari hizo ni zake. Katika kujibu hatua hiyo wizara ya ulinzi ya Taiwan ilisema kuwa imeimarisha mfumo wake wa ulinzi.

Japan pia ilisema kuwa makombora hayo ya China, yalianguka katika bahari inayomilikiwa na Japan, huku ikitoa wito wa kusitishwa na mazoezi hayo mara moja.

Also Read
Wakati China ikijitahidi kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, Marekani inadhuru maslahi ya nchi nyingine ili kujiendeleza

Ziara fupi ya Pelosi katika kisiwa cha Taiwan siku ya Jumatano, ilichochea taharuki, huku waziri wa mashauri ya nje wa Uchina Wang Yi akitaja ziara hiyo kuwa yenye uhasama. Pelosi ndiye afisa wa ngazi za juu zaidi kuzuru kisiwa cha Taiwan  katika muda wa miaka 25 iliyopita.

Also Read
Rubani aliyepeleka Corona Taiwan afutwa kazi

Marekani haitambui Taiwan kirasmi na lakini imedumisha uhusiano dhabiti na kisiwa hicho. Marekani inasemekana kuuzia kisiwa hicho silaha za kujikinga.

  

Latest posts

Wetangula kuamua Alhamisi ni chama kipi kitashikilia wadhifa wa kiongozi wa wengi bungeni

Tom Mathinji

Kipchoge na Kipruto warejea nyumbani kutoka London

Dismas Otuke

Rais William Ruto ampokea Mpambe mpya

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi