Chipukeezy ateuliwa naibu mwenyekiti wa bodi ya NACADA

Victor Muasya maarufu kama Chipukeezy jana aliteuliwa kuwa naibu mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya kudhibiti na kuzuia matumizi ya mihadarati NACADA.

Mchekeshaji huyo ambaye amekuwa mwanachama wa bodi hiyo kwa muda, aliteuliwa kwa wadhifa huo kwenye mkutano uliofanyika Jumanne tarehe 23 mwezi machi mwaka 2021.

Anachukua nafasi ya Peterson Mwai ambaye alihudumu kwenye wadhifa huo hadi mwisho wa mwaka 2020.

Also Read
Nameless amkumbuka E - Sir

Mwenyekiti wa bodi hiyo Profesa Mabel Opanda Imbuga akitangaza uteuzi huo, alisema kwamba Chipukeezy atakuwa wa maana sana kwani anaingiana na vijana ambao ndio walengwa wa kampeni za NACADA.

Muasya alishukuru kwa uteuzi huo na kuahidi kutumia wadhifa wake mpya kuendeleza mipango ya kufaidi vijana na watoto kulingana na mpango makhsusi wa NACADA wa kuwapa matumaini vijana ambao wamejikuta kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Also Read
Akuku Danger Alazwa Hospitalini Tena

Jambo lingine ambalo aliahidi kufanya ni kushirikiana na wanachama wengine wa bodi hiyo kubuni mwongozo mwafaka wa utendakazi wao hasa wakati huu ambapo taifa linapambana na janga la virusi vya Corona.

Also Read
Ronaldinho sasa ni mwanamuziki

Chipukeezy alijipatia umaarufu kupitia kipindi cha uchekeshaji cha “Churchill Show” ambacho kinaongozwa na mchekeshaji Daniel Ndambuki maarufu kama Churchill, na baadaye akaanzisha miradi yake binafsi kama vile wakfu wa Chipukeezy, The Funny Truth na The Chipukeezy Show.

  

Latest posts

Willy Poze adinda kuwajumuisha wasanii kwenye lebel yake kwa kuhofia skendo

Dismas Otuke

Gavana Sakaja atangaza maonyesho ya kila mwaka Jijini Nairobi

Tom Mathinji

Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Afrika Mashariki kuandaliwa Burundi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi