Chipukeezy Kuanzisha Kipindi Mitandaoni

Mchekeshaji wa Kenya Vincent Mwasia Mutua maarufu kama Chipukeezy anapania kuanzisha kipindi cha mitandaoni. Akizungumza kwenye mahojiano, mchekeshaji huyo alisema kwamba anataka kuanzisha kipindi lakini hataki kifanane na kile cha “The Chipukeezy Show” ambacho kilikuwa kikionyeshwa kwenye runinga. Msanii huyo anasema hataki tena kufanya mahojiano kwani anahisi alihoji watu vya kutosha na sasa anataka kufanya jambo tofauti.

Also Read
Chipukeezy Asherehekea Siku Yake ya Kuzaliwa

Hata hivyo anaridhika kwamba aliyoyafanya kwenye kipindi chake cha runinga kwa miaka mitatu yalimsaidia kujenga ujasiri na kufahamu mengi na sasa anataka kuzamia nyanja tofauti. Chipukeezy anataka kipindi anachoandaa kisheheni vichekesho vya moja kwa moja yaani Stand Up Comedy pamoja na kejeli za watu maarufu almaarufu comedy roast.

Mchekeshaji huyo anarejelea kazi yake ambayo anaipenda baada ya mkataba wake wa kuhudumu kwenye bodi ya kuzuia na kudhibiti matumizi ya mihadarati NACADA kufikia mwisho na baada ya kuandaa ziara ya kufanya nchini Marekani ambapo yeye na wachekeshaji wengine waliandaa matamasha ya vichekesho.

Also Read
Ellen DeGeneres Anakili Makala ya Mwisho ya Kipindi Chake

Mwasia alichapisha picha ya pamoja na mchekeshaji mwenza Kartelo akitania kwamba alikuwa amekubali kuwa mgombea mwenza wake ikitizamiwa kwamba kwa siku chache zilizopita, wagombea urais na ugavana wamekuwa wakitangaza wagombea wenza. “Ilikuwa vizuri kuonana na wewe baada ya muda mrefu.” aliandika Chipukeezy chini ya picha hiyo. Kartelo alikuwa nguzo muhimu kwenye kipindi cha runinga cha Chipukeezy isijulikane ikiwa watakuwa pamoja tena kwenye kazi mpya anayopanga kuanzisha mitandaoni.

  

Latest posts

Hata Nikifa Wanangu Hawatateseka – Asema Akothee

Marion Bosire

Miaka 70 ya Uwepo wa Ukumbi wa Maonyesho ya Sanaa

Marion Bosire

Ringtone Atangaza Kwamba Ameacha Kuimba Nyimbo za Injili

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi