Chipukizi 13 waliotamba Olimpiki kushiriki mashindano ya dunia ya U 20 Nairobi

Chipukizi 13 walioshiriki michezo ya Olimpiki  mjini Tokyo Japan watashiriki makala ya 18 ya mashindano ya dunia kwa vijana wasozidi umri wa miaka 20 yatakayoandaliwa uwanjani Kasarani jijini Nairobi kati ya tarehe 17 na 22 mwezi huu.

Baadhi ya  washiriki hao ni Priscah Chesang wa Uganda katika mita 3000 aliyemaliza wa 15 katika mchujo wa mita 5000 akiwa na umri wa miaka 18 katika michezo ya Olimpiki.

Also Read
Omanyala Omurwa afuzu kwa nusu fainali ya mita 100 Olimpiki na kusawazisha rekodi ya kitaifa

Ditaji Kambundji aliye na umri wa miaka 19 kutoka Uswizi atakayeshiriki mita 100 kuruka viunzi baada ya kumaliza katika nafasi ya 8 kwenye mchujo wake wa Olimpiki mjini Tokyo.

Also Read
Chama cha Riadha Kenya chasitisha shughuli zote kwa wiki mbili kimwomboleza Agnes Jebet

Ni dadake mdogo wa  Mujinga Kambundji aliyeshinda  shaba ya dunia ya mita 200 mwaka 2019.

Mshiriki mwingine wa kuangaziwa katika mashindano ya dunia ni Silja Kosonen katika urushaji nyundo kutoka Finalnd aliye na umri wa miaka 17,Christine Mboma wa Namibia aliyenyakua fedha ya mita 200 mjini Tokyo maajuzi.

Also Read
Chipukizi wa Wakenya watetemesha mibabe Doha Diamond league

Washiriki wengine ni Tazana Kamanga wa Denmark katika mita 200,Lythe Pillay wa mita 400 monegasque Charlotte Afriat ,Diribe Welteji wa Ethiopa na pia  Imaobong Nse Uko kutoka Ngeria.

Kenya itaandaa mashindano hayo baina ya tarehe 17 na 22 mwezi huu katika uwanja wa Kasarani.

 

  

Latest posts

Wakenya Rotich na Tanui wavunja rekodi za Paris na Amsterderm Marathon

Dismas Otuke

Tusker waleweshwa nyumbani na Zamalek 1-0

Dismas Otuke

Tysa yasherekea miaka 20 ya kubadilisha vijana Kitale kupitia soka

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi