Chipukizi Emmanuel Kiplagat adhihirisha umahiri na kushinda mita 10,000

Chipukizi Emmanuel Kiplagat alidhihirisha ukakamavu wa kiwango cha juu na kushinda fainali ya pili ya mita 10000 siku ya Ijumaa katika siku ya pili ya mashindano ya mchujo wa awali wa Olimpiki katika uwanja wa taifa wa Nyayo.

Kiplagat ambaye alimaliza masomo ya kidato cha nne maajuzi  aliwapiku wenzake na kukata utepe  kwa dakika 28 na sekunde 28  nukta 2 huku Edward Cheserek mwenye makao yake nchini marekani akishinda mchujo wa pili kwa dakika 28 na sekunde 10  nukta 41  ukiwa muda wa kasi kati ya michujo yote.

Also Read
Kenya tayari kuandaa Safari Rally asema Rais Uhuru

Ushindi wa Kipalagat wa Ijumaa ni wa pili tatu kwa chipukizi huyo aliye na umri wa miaka 17 ,baada ya kushinda mbio za mita 3000 na 5000 kwenye mchujo wa kuchagua timu ya chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20  yaliyoandaliwa Nandi wikendi iliyopita.

Also Read
Tusker kukabiliana na CS Faxien Jumapili alasiri ugani Nyayo

Cheserek ameibuka wa kwanza kwa jumla kutoka michujo yote ya mita 10,000 akifuatwa na Collins Koros  huku Emmanuel  Kiplagat akimaliza wa tatu akifuatwa na Ronald Kirui wakati Isaac Kipsang akihitimisha tano bora.

Collins Kipruto aliongoza nusu fainali ya mita 800 kwa dakika 1 sekunde 45 nukta 84 akifuatwa na Edwin Melly kwa dakika 1 sekunde 46  nukta 33 wakati Jonathan Kitlit akiambulia  nafasi ya tatu kwa dakika 1 sekunde  46  nukta 73.

Also Read
Peres Jepchirchir na Brigid Kosgei wanyakua dhahabu na fedha ya marathonpe

Maureen Thomas ameshinda fainali ya mita 200 kwa sekunde 23 nukta 69 akifuatwa na Monica Safania na Evangeline Makena katika nafasi za pili na tatu katika usanjari huo wakati Peter Mwai akiongoza upande wa wanaume kwa sekunde 20 nukta 85 akifuatwa na Samuel Chege  na Elijah Mathew katika nafasi za pili na tatu mtawalia.

 

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

KBC yafadhili timu ya magari itakayoshiriki mashindano ya Machakos Rallycross

DOtuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi