Chissano atoa wito wa mazungumzo kati ya serikali na wapiganaji

Aliyekuwa Rais wa Msumbiji Joaquim Chissano ametoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuzingatia kufanya mazungumzo na makundi ya wapiganaji katika eneo linalokabiliwa na vita ya Cabo Delgado.

Amesema kuna baadhi ya makundi ya kigaidi ambayo yameangamizwa kupitia mazungumzo.

Also Read
Watu 503 zaidi wathibitishwa kuwa na Covid-19 hapa nchini

Rais huyo wa zamani amesema kiini cha vita katika eneo la Cabo Delgado ni lazima kijulikane ili kumaliza vita hivyo.

Chissano amehudumu kama rais wa Msumbiji kutoka mwaka wa 1986 na 2005. Aliongoza mazungumzo yaliofanikiwa na kundi la waasi la Renamo ambayo yalipelekea kusitishwa kwa vita vilivyodumu kwa muda wa miaka 16, mnamo mwaka wa 1992.

Also Read
Uchukuzi wa umma watakiwa kuzingatia masharti ya kudhibiti Covid-19

Rais wa sasa Filipe Nyusi, ameelezea kujitolea kwake kufanya mazungumzo na makundi hayo ya wapiganaji, lakini akalalamika kwamba makundi hayo hayajaelezea kilichopelekea kuanzisha vita hivyo.

Also Read
Wizara ya afya yatahadharisha kuzuka kwa ugonjwa wa ukambi hapa nchini

Mkoa Cabo Delgado umekumbwa na vita tangu mwaka wa 2017, huku baadhi ya mashambulizi yakidaiwa kutekelezwa na kundili la kigaidi la Islamic State.

Tayari watu 3,000 wameuawa huku wengine 800,000 wakiachwa bila makao.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi