Chloe X Halle watangazwa mabalozi wa bidhaa za Neutrogena

Chloe Bailey na Halle Bailey, ni dada wawili ambao ni waimbaji na waigizaji nchini Marekani na katika muziki wanafanya kazi pamoja kama kundi liitwalo “Chloe x Halle”.

Wawili hao wamepatiwa kazi ya kuwa mabalozi wa bidhaa za urembo za Neutrogena na nyuso zao pia zitatumika katika kutangaza bidhaa hizo.

Kina dada hao walikuwa wakihojiwa ambapo walifichua habari hizo na kuongeza kwamba wana furaha ajabu kuhusishwa na bidhaa ambazo wamekuwa wakitumia.

Also Read
Tina Knowles-Lawson amkashifu Piers Morgan

“Walipotujia tulifurahi sana kwa kuwa sisi ndio dada wawili ambao wamewahi kufanya kazi ya ubalozi kwa pamoja na ninafurahia kuifanya kazi hii na rafiki wa dhati.” alielezea Chloe wa umri wa miaka 22 ambaye ndiye mkubwa.

Dogo Halle naye aliongeza kusema kwamba kauli mbiu ya bidhaa za Neutrogena imekuwa ” kuwa wewe halisi na kuacha undani wako ung’ae” na hilo ndilo jambo ambalo yeye na dadake wamekuwa wakitamani kuafikia maishani.

Also Read
Vanessa Williams azungumzia changamoto alizopitia

Wawili hao walitangaza habari hizo pia kupitia akaunti yao ya pamoja ya Instagram.

Maajuzi Chloe amesemwa sana kwenye mitandao ya kijamii baada ya baba mzazi wa Beyonce, Matthew Knowles, kukana maoni ya wale ambao wanamfananisha na binti yake.

Mzee huyo alikubali kwamba Chloe anaweza kuigiza kama Beyonce wa umri mdogo ikiwa atahitajika kufanya hivyo lakini akasema talata yake bado haijafikia ile ya Beyonce.

Chloe na Halle wamesajiliwa na kampuni ya muziki ya Beyonce ambayo inaitwa Parkwood Entertainment.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi