Cicely Tyson ameaga dunia

Muigizaji mkongwe wa nchi ya Marekani na filamu za Hollywood Cicely Tyson ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 96. Kifo chake kilitokea Alhamisi tarehe 28 mwezi Januari mwaka 2021 kulingana na saa za nchi ya Marekani.

Meneja wake wa muda mrefu Larry Thompson alithibitishia shirika la habari la CNN bahari hizo bila kutaja kilichosababisha kifo chake.

Cicely alisimulia safari yake ndefu ya uigizaji kwenye kitabu alichikipa mada “Just As I Am” ambacho kilizinduliwa jumanne wiki hii, siku chache kabla ya kifo chake.

Also Read
Christian Coleman Arejea kwa Kishindo

Tyson aliwakilisha vyema wanawake wamarekani weusi ambao walitaka kutambuliwa na kuheshimiwa kupitia kwa majukumu kadhaa ya uigizaji ambayo alitekeleza.

Aliigiza kama mama, kama aliyekuwa mtumwa,akaigiza kama mtetezi wa haki za binadamu kati ya kazi nyingine nyingi ambazo alitimiza.

Also Read
Tuzo za waigizaji wa vipindi vya runinga na filamu Marekani

Baadhi ya filamu ambazo aliigiza ni, “Sounder” ya mwaka 1972, “The Autobiography of Miss Jane Pittman” ya mwaka 1974, “Roots” ya mwaka 1977, “The Marva Collins Story” ya mwaka 1981, “The Women of Brewster Place” ya mwaka 1989 na “The Help” ya mwaka 2011.

Hata baada ya kuafikia ufanisi huo katika uigizaji, kuu kwake lilikuwa kuvishwa nishani ya uhuru na Rais Barack Obama mwaka 2016.

Also Read
"Wife Material itakuwa kubwa na bora zaidi" asema Eric Omondi

Alisema kwamba ni jambo kubwa sana kwake ikikumbukwa kwamba alilelewa eneo la mashariki la New York, sehemu iitwayo El Barrio na kutokea huko mpaka kufika ikulu ya White House kukaribishwa na Rais wa kwanza mweusi na kuvishwa medali ni fahari kubwa.

Cicely Tyson alizaliwa tarehe 19 mwezi Disemba mwaka 1924, huko New York.

  

Latest posts

Filamu ya Kenya yashinda tuzo nchini Nigeria

Tom Mathinji

Just A Band yarejea tena baada ya kimya cha muda

Tom Mathinji

Yul Edochie Azungumzia Ndoa Yake ya Wake Wawili

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi