Claude Makelele Kujenga Uwanja wa Soka Nyumbani Congo

Claude Makelele ni mcheza soka wa zamani ambaye aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa kwa miaka 13. Alicheza pia kwenye timu kama vile Paris Saint-Germain, Nantes, Marseille, Celta Vigo, Real Madrid na Chelsea na sasa anajihusisha na maswala ya ukufunzi wa soka. Mzaliwa huyo wa Congo ametangaza kwamba ana mpango wa kujenga uwanja wa soka katika mji wa Goma kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Also Read
Harambee Starlets kumenyana na Uganda Februari mwaka ujao kubaini ikiwa watatinga AWCON

Kulingana na mipango ya mapema, uwanja huo utakuwa na uwezo wa kukaliwa na mashabili elfu 58 kwa wakati mmoja na maegesho ya magari yenye uwezo wa kusheheni magari 300 kwa wakati mmoja. Shughuli ya ujenzi inatarajiwa kung’oa nanga mwaka ujao wa 2023.

Makelele alizaliwa nchini Congo mwaka 1973 kisha akahamia Ufaransa akiwa na umri wa miaka minne tu kwa ajili ya kujinoa kama mcheza soka. Haya yalitokana na uamuzi wa babake André-Joseph Makélélé, ambaye alikuwa mchezaji soka aliyewakilisha taifa lake la Dr Congo. akiwa na umri wa miaka 15 Claude alijiunga na klabu ya Sporting Melun-Dammarie 77 ambako alicheza kwa mwaka mmoja na kisha kuhamia kituo cha ukufunzi wa soka katika eneo la Brittany.

Also Read
Chelsea iliongoza kwa kutumia hela nyingi kwa usajili wachezaji

Mwezi Disemba mwaka of 1991, Claude ambaye alikuwa na umri wa miaka 18 alisajiliwa na FC Nantes na hapo ndipo alianza kuona matunda ya bidii yake ya mazoezi. Alijumuishwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo muda mfupi baada ya kusajiliwa kwani mmoja wa wasimamizi wa Nantes Robert Budzynski, alikuwa ashaona uwezo wake hata kabla ya kumsajili.

Also Read
Rais Wa Urusi Ashauriwa Kufanya Mazungumzo Na Mwenzake wa Ukraine

Safari ya mchezaji huyo wa zamani wa soka imekuwa nzuri na alistaafu kama mcheza soka mwaka 2011 akiwa na umri wa miaka 38.

  

Latest posts

Shikanda ahifadhi uenyekiti wa AFC Leopards

Dismas Otuke

Kalle Rovanpera atwaa ubingwa wa raundi ya Kenya mashindano ya WRC

Tom Mathinji

Peter Wahome na Fridah Chepkite washinda Lewa Marathon

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi