COVID-19: Kenya yanakili maambukizi mapya 705

Kiwango cha maambukizi ya virusi vya korona humu nchini kimefikia asilimia 8 baada ya Wizara ya Afya kuripoti visa vipya 705 kutokana na sampuli 8,853 zilizopimwa saa 24 zilizopita.

Kati ya visa hivyo vipya, 687 ni vya Wakenya ilhali 18 ni raia wa kigeni, wanaume wakiwa 404 na wanawake 301 kati ya umri wa mwezi mmoja hadi miaka 100.

Also Read
DCI yawaonya wanawake dhidi ya walaghai mitandaoni

Jumla ya visa vilivyothibitishwa imeongezeka hadi 162,098 baada ya jumla ya sampuli 1,701,385 kufanyiwa uchunguzi tangu mwezi Machi mwaka uliopita.

Wizara hiyo pia imethibitisha kupona kwa wagonjwa 711 wamepona kutokana na COVID-19 na kuongeza idadi ya waliopona hadi 110,480.

Kati ya hao waliopona leo, 412 walikuwa katika mpango wa kuwahudumia wagonjwa nyumbani, nao 299 wakiruhusiwa kuondoka kutoka vituo mbali mbali vya afya humu nchini.

Also Read
Wakristo waadhimisha Pasaka katika Mazingira tofauti

Hata hivyo, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ameripoti kuwa wagonjwa 25 wa COVID-19 wameaga dunia. Kufikia sasa jumla ya wagonjwa 2,850 wameaga dunia tangu kuwasili kwa virusi hivyo humu nchini.

Hadi sasa, wagonjwa 1,086 wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini huku 6,831 wakiwa chini ya utunzi wa nyumbani. Wagonjwa 131 wamelazwa katika wodi za wagonjwa mahututi, 28 kati yao wakiwa wanatumia vipumulio na 83 wakipokea hewa ya oksijeni.

Also Read
Magoha afutilia mbali uwezekano wa shule kufungwa tena

Kufikia sasa Wizara ya Afya imefanikiwa kuwachanja jumla ya watu 906,746 dhidi ya ugonjwa huo tangu shughuli hiyo izinduliwe, 528,615 kati yao wakiwa na umri wa miaka 58 au zaidi.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi