COVID-19: Kenya yanakili visa vipya 72 vya maambukizi

Kenya imenakili visa 72 vipya vya maambukizi ya virusi vya korona baada ya kupimwa kwa sampuli 2,056 katika muda wa saa 24 zilizopita, kiwango cha maambukizi kikiwa asilimia 3.5.

Hii inafikisha idadi jumla ya visa vilivyodhibitishwa vya maambukizi nchini kuwa watu 165,537 baada ya kupimwa kwa jumla ya sampuli milioni 1,746,449.

Kati ya visa hivyo vipya, watu 63 walikuwa raia wa Kenya huku tisa wakiwa raia wa kigeni. Watu 45 walikuwa wanaume huku 27 wakiwa wanawake.

Also Read
Visa 618 zaidi vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Mgonjwa mchanga zaidi alikuwa mtoto wa umri wa mwaka mmoja, huku mkongwe zaidi akiwa na umri wa miaka 84.

Wagonjwa 262 walipona ugonjwa huo, 235 wakiwa wale waliokuwa wakitibiwa nyumbani na 27 wakitoka katika hospitali mbali mbali nchini.

Idadi jumla ya watu waliopona nchini kwa sasa ni watu 113,874. Kati ya hao, 82,777 walipona kutoka mpango wa utunzaji wa nyumbani, huku 31,097 wakipona kutoka vituo mbali mbali vya afya.

Also Read
Mshukiwa wa mauaji ya watu watano wa familia moja Kiambu aungama

Watu 10 waliripotiwa kufariki na kufanya idadi jumla ya watu waliofariki kutokana na virusi hivyo vya corona kuwa watu 3,013.

Kulingana na taarifa ya Wizara ya Afya, jumla ya wagonjwa 1,036 wanaougua ugonjwa wa COVID-19 wanapokea matibabu katika vituo mbali mbali vya afya humu nchini, huku wengine 4,729 wako katika mpango wa kutibiwa nyumbani.

Also Read
Serikali yapiga marufuku uagizaji kibinafsi wa chanjo dhidi ya Covid-19

Kati ya wale walio katika vituo vya afya, 108 wako katika vitengo vya wagonjwa mahututi, 23 kati yao wakiwekewa vipumulio na 70 wakipokea hewa ya ziada ya oksijeni.

  

Latest posts

Mutahi Kagwe: Wahudumu wa afya wafeli katika somo la Kingereza

Tom Mathinji

Prof Magoha: Awamu ya kwanza ya ujenzi wa madarasa ya CBC kukamilika mwezi Aprili mwakani

Tom Mathinji

Benki ya dunia kuipa Kenya shilingi bilioni 16.7 kukabilia na ukame

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi