COVID-19: Watu 302 zaidi waambukizwa huku wagonjwa 17 wakifariki

Kenya imeripoti visa 302 vya maambukizi ya COVID-19 kutokana na upimaji wa sampuli 3,038 katika muda wa masaa 24 yaliyopita.

Jumla ya visa sasa vimefika 83,618 na jumla ya sampuli zilizofanyiwa uchunguzi kufikia sasa ni 888,971.

Visa hivyo vipya vinajumuisha Wakenya 286 na raia wa kigeni 191 ambapo 191 kati yao ni wanaume na 111 ni wanawake, kati ya umri wa mwaka mmoja hadi miaka 83.

Wagonjwa 369 wamepona leo kutokana na ugonjwa huo, 287 kutoka kwa mpango wa kuhudumiwa nyumbani na 82 kutoka hospitalini. Jumla ya waliopona humu nchini imefikia 55,344.

Also Read
NCIC yapiga marufuku utumiaji wa maneno yanayokisiwa kuwa ya uchochezi

Wagonjwa 17 pia wamethibitishwa kuaga dunia na kuifanya idadi ya maafa humu nchini kufikia 1,469.

Kulingana na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, jumla ya wagonjwa 1,282 wanapokea matibabu katika vituo mbali mbali vya afya kote nchini huku 8,405 wakihudumiwa nyumbani.

Wagonjwa 72 wako kwenye vyumba vya wagonjwa mahututi, 47 wakiwa kwenye vifaa vya kusaidia kupumua na 23 wanapokea hewa ya ziada ya Oksijeni.

Also Read
Bunge la Seneti kujadili hotuba ya Rais

Wakati uo huo, mkutano wa kamati ya kitaifa ya kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 ulioongozwa na Rais Uhuru Kenyatta umetoa pendekezo kwamba majukumu ya kamati hiyo yapanuliwe hadi katika maswala ya kutafuta chanjo dhidi ya ugonjwa huo.

Kwenye mkutano huo, kamati hiyo imepewa ripoti kutoka Shirika la KEMRI-Wellcome Trust, kuhusu utafiti unaoendelea kwa ushirikiano kati ya shirika hilo, Astra-Zeneca na Chuo Kikuu cha Oxford.

Also Read
Mshukiwa wa ulanguzi wa binadamu akamatwa Kisii

Kenya, kupitia kwa shirika hilo la utafiti, ni mojawapo kati ya nchi saba duniani zinazoshiriki katika utafiti wa Astra-Zeneca na Chuo Kikuu cha Oxford, wa kutengeneza chanjo dhidi ya COVID-19.

Waziri Kagwe amefichua kwamba jumla ya watu 60,000 wamejitolea kushiriki katika majaribio ya chanjo hiyo kabla mwisho wa mwaka huu.

“Huku KEMRI ikiendelea kushirikiana na Astra-Zeneca na Chuo Kikuu cha Oxford kwenye majaribio ya chanjo hii, serikali inaendelea kutafuta ushirikiano katika nafasi zenginezo,” akasema Kagwe.

  

Latest posts

IEBC yachapisha majina ya wagombea huru 38 wa Urais kwa gazeti la Serikali

Tom Mathinji

Kenya imenakili visa 26 vipya vya Covid-19

Tom Mathinji

Rais Kenyatta: Mataifa ya Afrika Sharti yakabiliane kikamilifu na zimwi la Ufisadi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi