COVID-19: Watu 427 zaidi waambukizwa huku mgonjwa mmoja akiaga dunia

Wizara ya Afya imethibitisha visa vipya 427 vya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 kutokana na upimaji wa sampuli 7,593 katika muda wa masaa 24 yaliyopita.

Visa hivyo vimefikisha jumla ya maambukizi humu nchini hadi 95,195 baada ya jumla ya sampuli 1,021,880 kufanyiwa uchunguzi tangu kisa cha kwanza kuthibitishwa humu nchini mwezi Machi.

Also Read
Haji akariri kwamba wahusika wa kashfa ya KEMSA watachukuliwa hatua

Kati ya visa hivyo, 406 ni vya Wakenya ilhali 21 ni raia wa kigeni, 256 kati yao wakiwa ni wanaume nao 171 ni wanawake, wote wa kati ya umri wa miaka mitano hadi 87.

Wizara hiyo pia imethibitisha kupona kwa wagonjwa 286. Kati ya hao, 228 walikuwa kwenye mpango wa kuhudumiwa nyumbani ilhali 58 walikuwa wakitibiwa hospitalini.

Also Read
Visa 1,561 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Hii imefanya idadi ya waliopona kuwa 76,508.

Hata hivyo, mgonjwa mmoja amefariki kutokana na makali ya COVID-19 na kuifanya jumla ya waliofariki humu nchini kuwa 1,648.

Also Read
Kenya yanakili visa 521 vipya vya Covid-19 huku watu 14 zaidi wakifariki

Hadi sasa, jumla ya wagonjwa 789 wanatibiwa katika vituo mbali mbali vya afya humu nchini nao 3,705 wanahudumiwa nyumbani.

Wagonjwa 43 wako kwenye vyumba vya wagonjwa mahututi, 20 kati yao wakiwa wanasaidiwa kupumua huku 21 wakiwa wanapokea hewa ya ziada ya Oksijeni.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi