Daniel Kaluuya – Mganda aliyeng’aa kwenye tuzo za Oscar

Daniel Kaluuya ndiye mshindi wa tuzo la muigizaji msaidizi bora wa kiume yaani “best supporting actor” kwenye tuzo za Oscar awamu ya 93.

Jukumu lake kama “Fred Hampton” kwenye filamu ijulikanayo kama “Judas and the Black Messiah” ndilo lilimshindia tuzo hilo.

Filamu hiyo imeelekezwa na Shaka King, na inaangazia jinsi Fred Hampton anasalitiwa na mpelelezi mmoja wa Shirika la Ujasusi la Marekani FBI William O’Neal.

Also Read
Mwalimu akatazwa kufunza chekechea kwa sababu ya "tattoo"

Kaluuya ameigiza pia kwenye filamu za “Widows” na “Black Panther” na kazi yake ijayo ni filamu ya matukio halisi yenye misingi ya kipindi cha watoto “Barney & Friends”. Yeye ndiye mtayarishaji wa kazi hiyo ambayo anasema itashangaza wengi na kugeuza matarajio yao.

Alizaliwa huko Uingereza tarehe 24 mwezi Februari mwaka 1989 lakini wazazi wake ni wazaliwa wa Uganda. Mamake ambaye anaitwa “Damalie” alimlelea katika makazi ya serikali ya wilaya ya Camden Town, jijini London Uingereza huku babake akichagua kusalia nchini Uganda.

Also Read
Maxine Waters asifia wimbo tatanishi

Daniel alikutana na babake kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 15 na ana dada mmoja.

Muigizaji huyo alimshukuru Mungu kwa ufanisi ambao amepata katika fani ya uigizaji huku akishukuru watu alioigiza kama vile Fred Hampton.

Also Read
Ada Ameh afiwa na mwanawe wa kipekee

Umaarufu wake ulijiri baada ya kuigiza kwenye filamu iitwayo “Get Out” yake Jordan Peele.

Alimaliza hotuba yake ya kukubali tuzo hilo na maneno ambayo yaliacha mamake ambaye alikuwa ukumbini na aibu usoni ambapo alisema wazazi wake walishiriki tendo la ndoa na sasa yeye yuko hapa.

  

Latest posts

Waigizaji Wa Nollywood Wazuru Zanzibar kwa Fungate

Marion Bosire

Betty Kyallo Apata Kazi ya Kuigiza

Marion Bosire

Gurdian Angel Asifia Mpenzi Wake

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi