David Major arejea kutoka “Rehab”

Mwanamuziki David Major alitikisa mitandao ya kijamii mwezi Novemba mwaka jana baada ya picha zake kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

David ambaye alikuwa mmoja wa washindani kwenye Tusker Project Fame, alionekana kuzidiwa na utumizi wa madawa ya kulevya na alikuwa bila makazi na alionekana mchafu kweli kweli kwenye picha hizo.

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii walijitolea kumsaidia kwa kuchangisha pesa ambazo zilitumiwa na mwanamuziki mwenza ambaye pia aliwahi kuwa kwenye Tusker Project Fame Alvan Gatitu kumpeleka kwenye kituo cha kurekebisha tabia kwa wanaotumia madawa ya kulevya.

Also Read
Juliani kuhutubia mhadhiri na wanafunzi wa chuo Kimoja huko Canada

Jana jioni, Alvan alipachika picha akiwa na David ambaye anaonekana tofauti kabisa akisema kwamba amerejea kutoka kwenye kituo hicho cha kurekebisha tabia yaani, “Rehab”. Alvan alikuwa mwingi wa furaha huku akimshukuru Mungu kwa kumbadilisha na kuonyesha imani kwamba ataendelea kumtengeneza.

David Major ni mtoto wa marehemu Dr. Margaret Ogola ambaye alikuwa Daktari, mwandishi maarufu wa vitabu na mtetezi wa haki za kibinadamu.

Dr. Ogola aambaye anafahamika sana kwa kitabu chake cha “The River and The Source” aliaga dunia mwaka 2011 baada ya kuugua saratani kwa muda.

Kitabu hicho kilitahiniwa kwenye fasihi ya kiingereza kwa mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE kati ya mwaka 1999 na 2004.

Tunamtakia David kila la heri anapojipanga kurejelea maisha ya kawaida.

  

Latest posts

Gurdian Angel Asifia Mpenzi Wake

Marion Bosire

Kibao Kipya cha Ringtone na Rose Muhando

Marion Bosire

Mulamwah Akaribisha Mwanawe

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi