DCI yaboresha kitengo chake cha uchunguzi wa mashamba

Idara ya upelelezi wa jinai imefanya mageuzi kwenye muundo wake katika juhudi za kuboresha kitengo cha uchunguzi wa wizi wa mashamba.

Kwenye baadhi ya mabadiliko hayo, jumla ya maafisa 26 walio na ujuzi wa kitaaluma katika usoroveya wa ardhi, uchumi wa ardhi uchoraji wa ardhi na usimamizi wataimarisha uwezo wa kitengo hicho katika kuchunguza kesi za ardhi na kutoa ushauri kuhusu hatua mwafaka ya kisheria inayohitaji kuchukuliwa.

Also Read
Ruto: Sitishwi na njama za mahasimu wangu

Kulingana na mkurugenzi wa idara ya DCI George Kinoti, hatua hiyo inanuia kuboresha kitengo hicho ili kiweze kuchunguza maswala tata kuhusu ardhi.

Kinoti alisema maafisa hao 26 walichaguliwa kwa makini zaidi na kusailiwa na kwamba wana tajiriba ya kuchunguza kesi sugu za ardhi.

Also Read
IEBC yahitaji shilingi bilioni 40 kuandaa uchaguzi Mkuu ujao

“Wataboresha uwezo wa kitengo hiki kuchunguza visa kuhusu ardhi kwa haraka na kushauri hatua za kisheria zitakazochukuliwa,”alisema Kinoti.

Haya yanajiri kabla ya kuanzishwa kwa mpango wa kutekeleza shughuli za ardhi kwa njia ya dijitali ambao utazinduliwa kwa uwiano na sheria ya mwaka 2012 kuhusu usajili wa ardhi.

Also Read
Viongozi wa Kiislamu Mombasa wahamimizwa kuhamasisha uzingativu wa kanuni za COVID-19 misikitini

Idara ya DCI imetoa wito kwa wananchi kupiga nambari ya simu 0800 722 203 na kutoa habari zozote kuhusu ardhi ili iweze kusaidia wananchi ipasavyo.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi