DCI yawakamata washukiwa wanaolaghai watu kwa kigezo cha kuwatafutia wapenzi

Maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Uhalifu nchini DCI wamewakamata washukiwa wanne wa kundi moja sugu la uhalifu huko Lang’ata, jijini Nairobi.

Wanachama wa kundi hilo wamekuwa wakiwahadaa watu wasio na habari kwenye mitandao ya kijamii kuwa wanawatafutia wapenzi na kisha kuwatesa na kuwapora pesa.

Kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter, maafisa wa shirika hilo wamesema washukiwa hao wanne walitiwa nguvuni jana jioni  katika kituo cha biashara cha Ruaka.

Also Read
Mwanajeshi akamatwa kwa kumshambulia mkewe kwa kilipuzi

Maafisa hao walivamia nyumba moja katika mtaa huo ambapo waliwafumania wahalifu wawili kwa majina ya Bernard Kivuva na Frederick Mutiso Mutua, wakimtesa raia mmoja kutoka Uturuki.

Mshukiwa wa tatu Catherine Mumbi Kivuva ambaye alimshawishi raia huyo wa Uturuki hadi nyumba hiyo kwa dai la kumtafutia rafiki kwenye mtandao pamoja na washukiwa wengine watatu pia walikamatwa.

Also Read
Wabunge washinikiza kuimarishwa kwa biashara kati ya Kenya na Tanzania

Mshukiwa wa nne Kelvin Nzioki ambaye alitiwa nguvuni huko Ruaka alipatikana na kadi za kutoa pesa  za benki ya Cooperative na alikuwa tayari kuzitumia kadi hizo kutoa pesa, baada ya kutoa pesa za raia huyo kutoka akaunti yake ya MPESA.

Imebainishwa kuwa Bernard Mbunga alikuwa akitafutwa na polisi baada ya kutoroka kutoka gereza moja baada ya kumpora raia mmoja wa kiHindi kwa njia hiyo katika mtaa wa Imara Daima.

Also Read
Mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Oyugi Ogango afariki dunia

Mashine moja ya benki ya Cooperative na rununu kadhaa zilinaswa kwenye msako huo.

Washukiwa wote wanasubiri kufikishwa mahakamani na kushitakiwa.

Raia huyo wa Uturuki alipelekwa hospitalini kupokea matibabu kufwatia kisa hicho.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi