DCI yawaonya wanafunzi dhidi ya utovu wa nidhamu shuleni

Mshukiwa mkuu katika kisa ambapo bweni la shule ya upili Kiambere liliteketezwa amekamatwa na maafisa wa idara ya upelelezi wa Jinai-DCI.

Mshukiwa huyo wa umri wa miaka 17 alikamatwa baada ya kutambuliwa na kisha akawataja wenzake 9 alioshiriki nao katika uteketezaji wa bweni hilo.

Wenzake waliokamatwa wana umri wa kati ya miaka 15 na 19.

Also Read
Mwanajeshi wa zamani akamatwa na barua feki za usajili wa KDF

Mkurugenzi mkuu wa idara ya upelelezi wa jinai George Kinoti amewatahadharisha wanafunzi wote humu nchini dhidi ya kushiriki kwenye migomo shuleni.

Kinoti alisema kufanya hivyo huenda kukawa na athari kubwa kwa maisha ya wanafunzi hao.

Kwenye taarifa, Kinoti alisema idara hiyo inaweka kumbukumbu ya mashtaka yote yanayoweza kuwakumba wanafunzi ambayo itajumuishwa kwenye cheti cha maadili kinachotolewa na idara ya polisi.

Also Read
Mwanabiashara wa Uturuki Harun Aydin arejeshwa kwao

Tahadhari ya Kinoti imewadia wakati ghasia na misukosuko zilishuhudiwa kwenye baadhi ya shule za humu nchini.

Kati ya siku ya Jumapili na Jumatatu asubuhi, ghasia pamoja na uharibifu wa mali zilishuhudiwa kwenye shule tano za humu nchini.

Also Read
Mwanaume aliyewajeruhi watu watatu katika baa ya Quivers afikishwa mahakamani

Kaunti ya Bungoma ndiyo iliyoshuhudia visa vingi zaidi ambapo cha hivi karibuni kilijiri kwenye shule ya upili ya wavulana ya St. Luke ambapo wanafunzi walivunja madirisha kadhaa kulalamikia hatua ya kiranja mmoja kumwadhibu mmoja wao.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi