Dhuluma za kimapenzi zapungua katika kaunti ya Makueni

Visa vya dhuluma za kimapenzi katika kaunti ya Makueni vimepungua pakubwa katika muda wa miaka miwili iliyopita.

Hayo yamesemwa na afisa mkuu wa polisi katika kaunti hiyo Joseph Ole Naipeyan.

Ole Naipeyan amesema jumla ya visa 157 vya unajisi viliripotiwa mwaka 2019 ikilinganishwa na visa  166 vilivyoripotiwa mwaka  2018.

Also Read
Wanafunzi 12 wakamatwa kwa kuteketeza bweni katika shule ya upili ya Mukaa

Visa  88 vimeripotiwa tangu mwezi Januari hadi sasa. Vile vile idadi ya visa vya ubakaji ilipungua katika kipindi sawia huku visa 27 vikiripotiwa mwaka 2019 ikilinganishwa na 35 mwaka  2018 huku visa 11 vikiwa vimeripotiwa hadi sasa mwaka huu.

Ole Naipeyan amesema waathiriwa wa unajisi ni wa kati ya umri wa miaka mitano na 17 na wale walioripoti visa vya ubakaji walikuwa na umri wa kati ya umri wa miaka 18 na  80.

Also Read
Rais Kenyatta awasili Ukambani kukagua Miradi ya maendelo

Akiongea Ijumaa katika kituo cha polisi cha Makueni wakati wa uzinduzi wa afisi ya kushughulikia dhuluma za kimapenzi na kijinsia kwa jina ‘PoliceCare’, Ole Naipeyan alisema kupungua kwa visa hivyo kuliwezeshwa na uhamasishaji dhidi ya dhuluma za kimapenzi na kijinsia miongoni mwa wasichana na wanawake.

Also Read
Ruto akosoa ufufuzi wa kesi za ghasia za baada ya uchaguzi

Alisema afisi hiyo ambayo ni ya kwanza kuzinduliwa hapa nchini itasaidia kuripoti na kutayarisha visa vya dhuluma hizo huku ikidumisha hadhi ya waathiriwa na familia zao.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi