Diamond aelimisha wanamuziki kuhusu You Tube

Diamond Platnumz ambaye yuko nchini Afrika Kusini kwa sasa kwa ajili ya kukutana na kuwa na muda na watoto wake na mzazi mwenzake Zari Hassan ameamua kuelimisha umma kuhusu mtandao wa You Tube.

Mmiliki huyo wa kampuni ya muziki ya Wasafi Classic Baby WCB aliamua kuelezea ni kwa nini yeye na wanamuziki anaosimamia wanapendelea mtandao wa You Tube na kuhakikisha nyimbo zao zinatizamwa kwa wingi.

Also Read
Shakilla asema ana ujauzito wa Eric Omondi!!

Kulingana naye, mitazamo au ukipenda Views kwenye mtandao huo ni mauzo ya kazi iliyopachikwa humo na wala sio majivuno. Alielezea kwamba wimbo wake kwa jina “Waah” ambao amemshirikisha Koffi Olomide ulipofikisha ‘views’ milioni 39 na zaidi, alilipwa Euro 32,266.53 sawa na shilingi milioni 4.2 za Kenya.

Mwanamuziki huyo hata hivyo alifafanua kwamba sio kila wimbo utapata malipo sawia ukiwa na mitazamo sawa na hiyo kwani inategemea na nchi ambapo wimbo unatazamwa sana kwani katika nchi nyingine wenye biashara huwekeza kiasi kikubwa cha pesha kwenye matangazo ya biashara ambayo huwekwa kwenye nyimbo au video za You Tube huku wengine wakiwekeza kiasi kidogo.

Also Read
Super Unfair! Babu Tale azomewa na mwanawe.

Kazi kubwa kulingana naye ni kuhakikisha kwamba mwanamuziki anatoa wimbo mzuri ambao utavuma sana na ukivuma utatizamwa kwa wingi na hivyo msanii atapata kipato kikubwa.

Also Read
Emmanuel Ehumadu ashutumiwa kwa kukusanya pesa za mazishi ya Asuzu

Akizungumzia kiwango cha uzuri wa muziki kwa wasanii na ku trend au kuvuma alikuwa amepachika picha ya wimbo wa Mbosso uitwao Baikoko kwenye You Tube ambapo uko nambari moja kwa Trending au ukipenda kuvuma.

Diamond alifika nyumbani kwa Zari usiku kulingana na video kwenye Instagram Stories ambapo alishiriki chajio nao.

  

Latest posts

Rayvanny Kumtambulisha Msanii wa Kwanza NLM

Marion Bosire

Dulla Makabila Ajiondolea Lawama

Marion Bosire

Mwigizaji Atoa Ilani Kwa Rais Museveni

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi