Diamond ateuliwa kuwania tuzo la BET

Diamond Platnumz msanii wa Muziki wa Bongo Fleva ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa Wasafi media ameteuliwa kuwania tuzo la BET mwaka 2021 katika kitengo cha mwanamuziki bora wa kimataifa.

Wengine walioteuliwa kuwania tuzo katika kitengo hicho, au ukipenda anaoshindana nao ni Aya Nakamura na Youssoupha kutoka Ufaransa, Burna Boy na Wizkid wa Nigeria, Emicida wa Brazil, Headie One na Young T & Bugsey wa Uingereza .

Also Read
Rotimi asherehekea mapenzi, siku yake ya kuzaliwa

Diamond ndiye anawakilisha Afrika Mashariki kwenye tuzo hizo na ni mmoja wa wasanii watatu wa Afrika walioteuliwa wengine wakiwa Burna Boy na Wizkid wote wa Nigeria.

Katika tuzo za BET mwaka jana, Burna Boy aliibuka mshindi katika kitengo hicho cha mwanamuziki bora wa kimataifa.

Tamasha la tuzo za BET litaandaliwa Jumapili, tarehe 27 mwezi Juni mwaka huu wa 2021 katika ukumbi wa Microsoft huko Los Angeles California nchini Marekani.

Also Read
Mwanaume afariki baada ya kukamilisha mchezo

Watu wataruhusiwa kuhudhuria tamasha hilo lakini kwa sharti kwamba wawe wamepokea vipimo vyote viwili vya chanjo dhidi ya virusi vya Corona. Tukio hilo litapeperushwa pia moja kwa moja kwenye runinga.

Megan Thee Stallion na DaBaby wote wa Marekani ndio wameteuliwa kuwania tuzo za BET mwaka huu katika vitengo vingi ambavyo ni saba kila mmoja.

Also Read
Mejja amelishwa Kamote!

Mange Kimambi ambaye ni mkosoaji mkuu wa Diamond Platnumz, amempongeza kwa uteuzi huo lakini anahisi kwamba tuzo litakwenda Nigeria. Kuhusu utajiri na orodha ya Forbes ya wanamuziki tajiri zaidi barani Afrika, Mange aliamua kumwelezea Diamond ni kwa nini aliorodheshwa vile.

  

Latest posts

Rayvanny Kumtambulisha Msanii wa Kwanza NLM

Marion Bosire

Dulla Makabila Ajiondolea Lawama

Marion Bosire

Mwigizaji Atoa Ilani Kwa Rais Museveni

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi