Diamond Platnumz atia saini mkataba na Warner Music

Diamond Platnumz ametangaza kwamba ametia saini mkataba na kampuni ya muziki kwa jina Warner Music na nyingine ya Ziiki za Afrika Kusini.

Mkataba huo unajumulisha kampuni ya Diamond ya kusimamia wanamuziki ya Wasafi Classic Baby, WCB.

Warner Music, Diamond Platnumz, Ziiki Media na wasanii wa WCB watashirikiana katika kutoa nyimbo mpya, kuorodhesha nyimbo na mengine yanayohusu kazi ya muziki.

Also Read
Mwanamuziki wa Marekani Offset akamatwa na polisi

Diamond alisema alianzisha WCB mwenyewe na anaamini Warner Music na Ziiki ni washirika bora.

Kulingana naye mipango waliyonayo ni mizuri wanapojiandaa kupanua wigo wao.

Msimamizi wa kitengo cha masoko ibuka katika kampuni ya Warner Alfonso Perez-Soto, alikaribisha Diamond na kampuni yake akisema yeye ni mwanamuziki na mfanyibiashara mzuri.

Also Read
Teni alivyomfuata Davido usiku ili kupata Colabo!

Temi Adeniji ambaye ni mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Warner Music South Africa anaonelea kwamba makubaliano hayo ya ushirikiano ni ishara kwamba kampuni yake itaongeza wigo katika soko la muziki eneo la Afrika Mashariki.

Kampuni ya Ziiki Media, ambayo iliingia kwenye mkataba na Warner Music mwaka jana, nayo inatazamia ushirikiano mwema kikazi na Diamond Platnumz na Kundi lake.

Also Read
Sukari, Zuchu

Diamond alichapisha video fupi ambayo inamwonyesha yeye, meneja wake Babu Tale na wengine ambao wanaaminika kuwa wa kampuni za Warner na Ziiki wakipata kinywaji kama njia ya kusherehekea mkataba huo.

Haya yanajiri wakati ambapo Diamond ametupilia mbali orodha ya jarida la Forbes Africa ya wanamuziki tajiri barani Afrika.

  

Latest posts

Rayvanny Kumtambulisha Msanii wa Kwanza NLM

Marion Bosire

Dulla Makabila Ajiondolea Lawama

Marion Bosire

Mwigizaji Atoa Ilani Kwa Rais Museveni

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi