Diamond Platnumz kusambaza msaada leo

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Wasafi Diamond Platnumz, ametangaza kwamba atatoa alichojaliwa kama zawadi ya siku kuu ya Eid kwa watu wa eneo la Tandale alikozaliwa na kulelewa.

Zoezi hilo ambalo litafanyika leo baada ya sala ya Eid litasambazwa katika maeneo mengine ambapo atawakilishwa na ndugu na washirika wake wa karibu.

Also Read
Sai Kenya Akana Tetesi Kwamba Ameolewa

Diamond alitangaza hayo Kupitia Twitter akisema katika eneo la Kariakoo zoezi hilo litaongozwa na kakake kwa jina Ricardo Momo.

Ricardo ndiye alijulikanisha kupitia redio kwamba Mzee Abdul Juma hakuwa baba mzazi wa Diamond na kwamba yeye na Diamond ni watoto wa baba mmoja kwa jina Salum Nyange.

Also Read
Tuzo za Kalasha

Mkubwa Fella ambaye ni mmoja wa mameneja wa wasanii kwenye WCB, ataongoza shughuli hiyo ya kutoa zawadi ya Eid kwa niaba ya Diamond huko Kilungule huku mheshimiwa Babu Tale akiandaa zoezi sawia Morogoro Mkuyuni.

Mjomba wake Mrisho atakuwa anamsaidia Diamond kugawa zawadi hiyo ya Eid katika maeneo ya Kigoma, Ujiji, Buzebazeba mtaa wa Sokoine na atasaidiwa na watu wa familia yao ya mzee Bukuku.

Also Read
Baba Levo amshauri Shilole

Eid al Fitr ni siku kuu ya watu wa dini ya kiisilamu na ni ya kusherehekea kwa chakula kama njia ya kuvunja mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Inaashiria mwisho wa mwezi huo mtukufu.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi