Didmus Barasa Kufikishwa Mahakamani Leo

Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi leo baada ya kukaa kwenye korokoro za polisi huko Bungoma tangu Ijumaa. Barasa alijisalimisha kwa polisi kuhusu kisa ambapo alimpiga risasi Brian Olunga mlinzi wa mpinzani wake Brian Khaemba kwenye kituo cha kupigia kura cha Chebukwabi. Olunga aliaga dunia akipokea matibabu kutokana na jeraha la risasi kichwani.

Also Read
Watu wanne wafariki katika ajali ya barabarani Bungoma

Kiongozi huyo alitoweka punde baada ya kutekeleza kitendo hicho na maafisa wa vitengo mbali mbali vya usalama wakawa wanatoa wito kwake ajisalimishe. Kabla ya kujisalimisha wakili wa Didmus John Khaminwa alikuwa amekwenda mahakamani kutafuta maagizo ya kuzuia kukamatwa kwa mteja wake jambo ambalo inaonekana halikutimia.

Also Read
Didmus Barasa achaguliwa mbunge wa Kimilili kwa muhula wa pili

Msimamizi wa uchaguzi katika eneo bunge la Kimilili alimtangaza Barasa mshindi katika kinyang’anyiro cha ubunge bila uwepo wake kituoni na kakataa kukabidhi wakala wake cheti cha uteuzi.

Also Read
Kenya kuanzisha ukuzaji mahindi yaliyoboreshwa kwa mbinu ya kisayansi,GMO

Familia ya marehemu Olunga ilitoa wito kwa maafisa wa usalama kuharakisha uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya wahusika wa mauaji ya mpendwa wao.

  

Latest posts

Wetangula kuamua Alhamisi ni chama kipi kitashikilia wadhifa wa kiongozi wa wengi bungeni

Tom Mathinji

Gavana Orengo awatuma maafisa wakuu wa kaunti kwa likizo ya lazima

Tom Mathinji

Rais William Ruto ampokea Mpambe mpya

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi