Mabingwa watetezi wa ligi kuu Kenya, Tusker Fc wametangaza kuondoka kwa nahodha wao Eugine Asike amayetarajaiwa kujiunga na klabu ya Karlstad Fotboll nchini Sweden.
Asike aliye na umri wa miaka 28 anagura Tusker FC baada ya kuwachezea kwa miaka sita akinyakua ubingwa wa ligi kuu mara mbili na kombe moja la shirikisho.
Difenda huyo ambaye pia alitwaa tuzo ya beki bora wa mwaka anajiunga na idadi kubwa ya wanandinga wa Kenya katika ligi kuu ya Sweeden Henry Meja, Collins Sichenje na Eric Marcelo .