Kenya ni nchi iliyo na uhuru wa kuabudu kutokana na idadi kubwa ya dini na imani za kuabudu zinazopatikana na kukubaliwa .
Hii ni haki ya kimsingi kwa kila Mkenya inayopatikana katika katiba ya Kenya.
Wakristo ndio wengi nchini Kenya, huku zaidi ya nusu ya idadi ya watu kwa jumla wakiwa Wale Wakiprotestanti.
Kulingana na takwimu za mwaka 2019 zaidi ya asilimia 85 ya idadi ya Wakristo ilikuwa na asilimia 33 nukta 4 ya Waprotestanti,asilimia 20 nukta 4 wakiwa wa Evangelicals, na asimilia 7 kutoka taasisi ya makanisa.
Asilimia 11 ni Waislamu.
Kabla ya ujio wa dini makabila na watu mbali mbali walikuwa na imani tofauti huku asilimia ndogo wakiwa wale wasioamini Mungu.
Dini maarufu zaidi nchini Kenya ni ya Wakristo ingawa pia kuna dini za Kiislamu ,Kihindi na imani za tamaduni za Kiafrika.
Dini za Kikristo na Kiislamu zote zililetwa nchini na wageni wa kutoka nje ya nchi, Kiislamu kikiletwa na Waarabu huku ukristo ukiletwa na Wazungu wa ulaya.
Kabla ya ujio wa dini za Kikristo na Kiislamu , makabila ya Kenya yalikuwa na imani tofauti za kuabudu .
Baadhi ya imani zilizokuwa maarufu nchini Kenya za kuabudu ni kuamini kuwepo kwa mababu yaani ancestors,kuamini kuwepo kwa dunia na utoaji kafara.
Ingawa mila zimepungua bado kunayo asilimia ndogo ya wale wanaoamini itikadi hizi.
Licha ya uhuru wa kuabudu ulio kwenye katiba ya Kenya ,Waislamu wamekuwa wakilalama hukusu kunyimwa haki zao za kimsingi za kuabudu na serikali na kuleta mtafaruku baina ya Wakristo na Waislamu .
Hali hii imeletwa na baadhi ya Waislamu waliojiunga na makundi ya kigaidi na kulazimu serikali kukabiliana nayo vikali.
Dini la Kiprotestanti
Dini la kiprotestanti lilianzishwa katika karne ya 16 wakati mwanaharakati Martin Luther alipoongoza kugawanyika kwa kanisa la Katoliki la Roma nchini Ujerumani .
Waprotestanti wanafahamika kwa kupinga utawala mkubwa na kupewa nguvu nyingi kwa Papa mtakatifu katika dini la kikatoliki la Roma.

Idadi ya Waprotestanti ndio kubwa nchini kwa sasa miongoni mwa waumini wote, ikiwa na wafuasi takriban asilimia 47.7 ya Wakenya wote.
Dini hii ililetwa nchini na mmishonari wa Ujerumani John Ludwig Krapf, aliyewasili mwaka 1844.
Krapf ndiye aliandika Bibilia ya kwanza kwa lugha ya Kiswahili .
Wamishonari waliongezeka nchini enzi za utawala wa wakoloni na ndio waliochangia kuleta elimu na huduma za kisasa za afya.

Ni kwa sababu hii ambapo shule nyingi hapa nchini Kenya na hospitali nyingi zimejengwa na makanisa.
Madhehebu ya Kiprotestanti nchini ni kama vile kanisa la Kianglikana ,kanisa la Kipresibiteri ,kanisa la kimethodi,kanisa la Kibaptista ,kanisa la Lutherani na makanisa ya Kipentekote.
Kanisa Katoliki
Kanisa la Roman Catholics linajumuisha asilimia 23 nukta 4 ya idadi ya Wakenya wote.
Kanisa Katoliki lilianzishwa nchini kwa mara ya kwanza na Wareno katika karne ya 15, lakini lilianza kuenea katika karne ya 20 .
Kanisa Katoliki la Roma katika ukanda wa Afrika mashariki, lilianza kwa mkusanyiko wa Wafaransa waliokuwa na imani ya uwepo wa roho mtakatifu haswa miongoni mwa watumwa walioachiliwa huru katika eneo la pwani.
Kasisi Allgeyer anaaminika kuchukua hatua ya kwanza kueneza injili nchini .
Punde baada ya kujengwa kwa reli ya kwanza nchini mwaka wa 1899 ,Wamishonari wa Holy Ghost waliwasili wakifuatwa na wale wa Consolata Fathers mwaka 1902 na baade kuenea katika maeneo ya Kiambu, Limuru, Mang’u, Thika, Nyeri, na Meru.
Kanisa Katoliki ndilo linalomiliki mashamba mengi na mali nyingi nchini wakiwa na idadi kubwa ya shule na hata pia hospitali .
Makanisa ya kisas a yanakuwa na kuenea kwa haraka kuliko makanisa ya kale ya wamishonari.
Uislamu
Dini la Kiislamu lilianzishwa na mtume Muhammad huko Arabia .
Mafunzo yaje yanapatilana kwenya kitabu chao kitakatifu cha Quran .
Uislamu uliletwa nchini katika karne ya 18 na kwa sasa ina waumini asilimia 9 nukta 9 ya idadi yote ya watu.
Waislamu wengi nchini Kenya ni wa mrengo wa Sunni huku wachache wakiwa wa mrengo wa Shia.
Waislamu wengi Kenya wanapatikana pwani na kaskazini mashariki mwa taifa la Kenya.
Wasioamini Mungu
Kundi la wasioamani Mungu maarufu kama na Atheists pia lipo,na kundi la Atagnostics ambao hawaamini kuwepo wala kutokuwepo kwa Mungu wakisema kuwa haijulikani.
Watu hawa wanajumuisha asimilia 2 nukta 4 ya idadi ya watu nchini.
Imani za tamaduni za Kiafrika
Imani za tamaduni za Kiafrika pia zingalipo baadhi ya watu wakiamini uwepo wa mababu na miungu .
Hata hivyo ni asimilia 1 nujta 7 pekee ya Wakenya wanaomini tamaduni hizi miongoni mwao wakiwa wa kutoka mlima Kenya na Wamijikenda .
Imani nyinginezo.
Imani nyingine nchini Kenya ni kama Hinduism,Judaism na Buddhism.
Takriban asilimia 97 nukta 6 ya Wakenya wanaamini katika dini.
Kwa jumla kanisa la Kiprotestanti lina wafuasi asilimia 47 nukta 7,likifuatwa na Roman Catholic kwa asimilia 23 .4,Waislamu asilimia 12 ,wasioamini Mungu asilimia asilimia 2 nukta 4,tamaduni za Kiafrika asilimia 1 nukta 7 na wengine asilimia 1 nukta 8 wakiamini itikadi nyingine .