Dismus Barasa aachiliwa kwa dhamana ya shilingi 100,000

Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi  100,000 pesa taslimu na hakimu wa mahakama ya Kimilili Gladys Adhiambo.

Mbunge huyo alikamatwa akiwa nyumbani kwake huko Kimilili kaunti ya Bungoma Jumatatu alfajiri, na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Kimilili.

Also Read
Shule ya wasichana ya Lugulu yafungwa kufuatia ghasia za wanafunzi wanaolalamikia ubakaji

Barasa alikanusha mashtaka ya kumjeruhi mwanakandarasi mmoja aliyeshinikiza kulipwa deni lake baada ya kujenga madarasa matano katika shule ya msingi ya Baptist Lurare kwenye wadi ya Kamukuywa.

Mwanakandarasi huyo aliye pia mwanamuziki kwa jina Stephen Masinde, almaarufu Steve Kay anamshtumu mbunge huyo wa Kimilili kwa kumshambulia.

Also Read
JSC kuendelea na usaili wa wawaniaji wa nafasi ya Jaji Mkuu

Kwenye kanda ya video iliyoenea katika mitandao ya kijamii, Barasa anaonekana akibishana na mwanakndarasi huyo kabla ya kumzaba kofi.

Mbunge huyo alikuwa amewasili kwenye shule ya msingi ya Baptist Lurare katika eneo bunge lake, kuzindua madarasa yaliyojengwa kupitia hazina ya ustawi wa eneo bunge hilo lakini akapata yamefungwa.

Also Read
Serikali kuharamisha utumizi wa kahawa kama dhamana ya mikopo

Yadaiwa kwamba mwanakandarasi huyo alifunga madarasa hayo kushinikiza malipo ya shilingi milioni-3.4.

  

Latest posts

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Wabunge wa kaunti ya Kitui wataka baa la njaa kutangazwa janga la kitaifa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi