Dj Pinye Atimiza Umri wa Miaka 51

Mpiga muziki wa muda mrefu nchini Kenya Peter Chuani maarufu kama Dj Pinye ana kila sababu ya kutabasamu baada ya kutimiza umri wa miaka 51. Pinye anaandaa sherehe ya aina yake kwenye eneo la burudani la Carnivore jijini Nairobi Jumamosi tarehe 29 mwezi Januari mwaka 2022. Alichagua Carnivore kwa sababu hapo ndipo alianzia.

Katika mahojiano ambayo amekuwa akifanya kwa kujiandaa kwa siku hiyo, Pinye amefunguka kuhusu mambo mengi maishani mwake lakini kuu ambalo limeshangaza wengi ni kwamba hadi sasa hajaoa na hawazii kuoa.

Also Read
Gucci Mane asajili mwanamuziki mwingine

Alikiri pia kwamba hakuwahi kuwa na uhusiano mwema na mamake mzazi kwa sababu ya ukaidi wa ujana wakati huo kiasi cha kuchoma moto nyumba yao. Hata hivyo anasema alirekebisha uhusiano kati yake na mamake siku chache kabla ya kifo chake ambapo pia alimfichulia kwamba yeye ndiye alianzisha moto uliochoma nyumba yao.

Baada ya kifo cha mamake mzazi, Pinye aligundua ghafla kwamba alikuwa na jukumu kubwa la kutunza kakake ambaye alizaliwa na kupooza kwa ubongo yaani cerebral palsy lakini hakujua jinsi ya kutekeleza kazi ambayo mamake peke yake aliifahamu. “Ilibidi tuajiri wauguzi.” alielezea Pinye huku akisema kwamba kakake aliaga dunia siku chache baada ya kifo cha mama yao.

Also Read
Mwanamuziki T.I aondolewa kwenye filamu ya Ant-Man 3

Kuhusu kazi ya kupiga muziki, Dj Pinye anasema kwamba kazi hiyo imekuwa rahisi sikuhizi kutokana na vifaa vya uzuri wa hali ya juu na ujio wa mtandao ambapo wapiga muziki wanakutana na mashabiki wao bila shida.

Also Read
Mashabiki wa Diamond Platinumz walalamikia muda kidogo alipatiwa kwenye wimbo wa Alicia Keys

Alipotimiza umri wa miaka 45, Dj Pinye ambaye ni mndani yaani Introvert aliamua kustaafu kama mpiga muziki lakini miaka mitano baadaye akarejelea kazi hiyo kutokana na pengo lililosababishwa na janga la Corona ambalo lilisababisha sehemu za burudani kufungwa na hitaji la watu kupata burudani wakiwa nyumbani.

Hapo ndipo Dj Pinye alianzisha onyesho la kupiga muziki mitandaoni yaani “The Sunday Cruise Online show”.

  

Latest posts

Travis Scott Atoa Msaada wa Masomo kwa Wanafunzi 100

Marion Bosire

Nandy na Billnass Waendeleza Maandalizi ya Harusi

Marion Bosire

Chipukeezy Kuanzisha Kipindi Mitandaoni

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi