Dozi ya tatu dhidi ya COVID-19 Israel yaonyesha ufanisi

Mpango wa Israel wa kutoa dozi ya tatu ya chanjo dhidi ya COVID-19 kwa watu walio na umri wa miaka 40 na zaidi umeanza kudhihirisha ufanisi.

Hata hivyo ongezeko la hivi maajuzi la visa vya maambukizi nchini humo limeibua mjadala kuhusu hatima ya mpango huo wa utoaji chanjo na janga hilo linaloendelea.

Also Read
Bara la Afrika lasifiwa kwa kudhibiti Covid-19

Ilikuwa imerejelea maisha ya kawaida kufikia majira ya kuchipuza na ilionekana kana kwamba utoaji chanjo umedhibiti janga hilo kikamilifu. Hata hivyo kuanzia mwezi Julai visa vilianza kuongezeka tena.

Also Read
Hakuna kuwatembelea wagonjwa katika hospitali ya Nakuru level 5

Na kwa vile Israel ilitia juhudi za kuwapa chanjo raia wake katika majira yaliyopita ya baridi mataifa mengine duniani yanatathmini hali nchini humo ili kufahamu yatakayojiri katika majuma na miezi ijayo.

Also Read
Harambee Stars kufa kupona dhidi ya Mali mjini Agadir Alhamisi usiku

Viongozi wa sekta ya afya nchini humo watakuwa wakichunguza hali ya maambukizi baada ya shule kufunguliwa tena tarehe mosi mwezi huu ilhali juma lijalo wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa kiyahudi ya Rosh Hashanah, makundi ya watu watakusanyika.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi