Duale: Tutaunga mkono BBI ikiwa maslahi yetu yatatiliwa maanani

Mbunge wa Garissa mjini  Aden Duale amesema kuwa eneo hilo litaunga mkono mchakato wa kuleta maridhiano nchini-BBI iwapo ajenda ya marekebisho iliyoko katika ripoti hiyo itashughulikia matakwa yao.

Kwa mujibu wa Duale eneo hilo kama maeneo mengine nchini lina changamoto zake ambazo zinapaswa kushughulikiwa na ripoti hiyo.

Also Read
Waumini wa Kanisa la Shianda wahakikishiwa kufanyika kwa mchango wa Ruto

Duale ambaye ni mlezi wa kundi la wabunge wa kutoka eneo la kaskazini mashariki amesema kuwa wakazi wa eneo hilo wanafuatilia kwa makini mjadala huo wa BBI na wana hamu ya kujua kitakachokuwa katika ripoti ya mwisho kabla ya kufanya uamuzi wao.

Also Read
Philip Murgor apigwa msasa kwa wadhifa wa Jaji Mkuu

“Nimekuwa nikifuatilia swala hili kwa makini na tutaunga mkono ajenda ya  maridhiano iwapo maslahi ya waislamu yatatiliwa maanani,” alisema Duale.

Kuhusu swala la jaji mkuu kumshauri rais kuvunja bunge, Duale alisema kuwa Maraga hawezi kuwalazimisha wakenya kuwachagua wanawake.

Also Read
Zoezi la kuchanja mifugo kwa wingi lang’oa nanga Garissa

Alisema kuwa iwapo rais atatimiza ushauri wa jaji mkuu na kuvunja bunge, hakuna kitakachobadilika.

Wakati alipokuwa kiongozi wa wengi bungeni,  Duale alijaribu kuhakikisha kuwa mswada huo unapitishwa bila mafanikio.

 

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi