Dulla Makabila Ajiondolea Lawama

Msanii wa muziki aina ya Singeli nchini Tanzania, Dulla Makabila ametangaza kwamba baba mzazi wa mtoto aliyesingiziwa amejitokeza.

Makabila alipachika picha ya mtoto huyo, jamaa anayesemekana kuwa babake na yake kwenye Instagram na kuandika maneno haya, “Miezi kadhaa nyuma, nilionekana mwanaume mpumbavu ambaye anaikataa damu yake na wengine wakahisi nakataa mimba kwa kuhofia kuvunja ndoa yangu jambo ambalo liliwakera mashabiki zangu hasa wa kike ambao walivaa Kiatu cha binti alosema ana mimba yangu.”

Also Read
Nandy atoa nyimbo za Injili

Mwanamuziki huyo anaelezea kwamba Kuna jamaa mmoja ambaye anajiita “@byorderog” kwenye Instagram alimtafuta ili kumthibitishia kwamba yeye ndiye baba mzazi wa mtoto ambaye alizaliwa na yule binti.

Also Read
Harambee Stars kupimana ubabe na Taifa Stars Jumatatu alasiri

Ithibati alizopatiwa Dulla ni pamoja na jumbe fupi kwenye simu ya rununu na sauti za mawasiliano kati ya @byorderog na mwanadada huyo kama wapenzi.

Dulla ambaye alifunga ndoa na mke wake Rahima mwisho wa mwezi Mei mwaka huu wa 2021, anasema kisa cha kusemekana kutunga mwanadada huyo mimba na Kisha kumkana kilimsababishia matatizo kati yake na ndugu zake.

Also Read
Kenya kupambana na Uganda nusu fainali ya CECAFA Jumatatu
Dulla na Rahima

Kwa sasa anasema ikiwa msichana huyo ataendelea kumhusisha na mtoto huyo itabidi agharamie vipimo vya DNA ili kufahamu ukweli thabiti.

Gwiji huyo wa mtindo wa singeli Sasa anataka apatiwe muda azingatie ndoa yake halali ili naye apate mtoto wa halali.

  

Latest posts

Ogopa Wasanii, Kibao Kipya Cha Willy Paul

Marion Bosire

Kipindi Cha Wendy Williams Kuendelezwa na Watangazaji Tofauti

Marion Bosire

“Upendo” Kibao Kipya Kutoka Kwa Zuchu Na Spice Diana

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi