EACC kuwahoji maafisa wa KPLC kuhusu kasoro za ununuzi

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC imewaita maafisa tisa wa kampuni ya usambazaji umeme Kenya Power kuandikisha taarifa kutokana na hali ya kuvurugwa kwa taratibu za ununuzi wa bidhaa.

Also Read
Sonko mashakani huku hoja ya kumbandua ikiwasilishwa katika bunge la kaunti ya Nairobi

Kwenye taarifa , tume hiyo imesema maafisa hao tisa ambao wote ni wanachama wa bodi ya wakurugenzi ya kampuni hiyo ya KPLC wanafaa kufika katika jumba la Integrity Center ili kuhojiwa.

Mwezi Agosti mwaka 2021, zabuni ya kampuni hiyo ya mawakala wa bima ilisimamishwa kwa muda kufuatia agizo lililotolewa na jaji James Makau baada ya kuombwa kufanya hivyo na mwanaharakati Okiya Omtatah.

Also Read
Mvua kubwa inatarajiwa siku ya Ijumaa hapa nchini

Jaji Makau aidha aliidhinisha kesi hiyo ya Omtatah kuwa ya dharura na akaagiza kuwa Omtata awakabidhi wahusika stakabadhi zake za kesi katika muda wa siku nne. Kesi hiyo itatajwa tarehe 22 mwezi Septemba.

  

Latest posts

Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 200,000 za Sinopharm kutoka China

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi